tanga 2014 gazeti

12
ISSN-1821-8946 TOLEO LA 7 - FEBRUARI, 24-1 MACHI, 2014 BEI. SH.500 Pembe Mills kuweka matangazo Mkwakwani SAUTI YA TANGA UK.11 Coming together is a Beginning Keeping together is Progress Working together is Sucess CONTACTS: HEAD OFFICE: Whole sale & Retail Jamhuri St. Sub-Whole Sale: 14 Sikukuu Msimbazi St. BRANCH: Haidery Plaza / Ground Floor. ADDRESS: P.o. Box 20073, DSM - TEL: 2117090 / 2117358 FAX: 2117357 MOBILE: 0713 325488 E-MAIL: [email protected] For all your school and office requirement PRIDE OF THE NATION SIMBA CEMENT SIMBA CEMENT REGISTERED OFFICE Tanga Cement Company Limited Korogwe Road, Pongwe Factory Area P.o. Box 5053, Tanga Tanzania Tel: + 255 27 2644500 - 2/2610604 Mob: + 255 784 644500 Fax: + 255 272646148 Website:www.simbacement.co.tz DAR ES SALAAM OFFICE: 3rd Floor, Coco Plaza, 254 Toure Drive p.o. Box 78478, Dar es Salaam, Tanzania Tel. + 255 22 2602778-9/2602784 Mob: + 255 685 602784 Fax: + 255 22 2602785 Email: [email protected] Pongwe City mji mpya wa Tanga Ijue Pongwe City uk.3 Uwanja wa Mkwakwani uk.11 Redio za Tanga uk.2 Na Wiliam Mngazija K ATIKA kile ambacho kinaonekana ya kuwa uongozi wa mkoa wa tanga na jiji hawataki kuharibu mandhari ya jiji la Tanga wameamua ya kuwa ni vyema wajenge mji mpya ili kuacha mandhari ya jiji la Tanga ibaki kama ilivyo. Kitendo hiki ambacho kimeafanywa na mkoa wa Tanga na uongozi wa jiji ni cha kupongezwa kwani mpaka hivi sasa mji wa Tanga ni kati ya miji ambayo inasifika kwa kuwa na mandhari yake halisi.Jiji la Tanga limepangika vizuri bado utakuta kuna mitaa ya kutoka barabara ya kwanza mpaka ya ishirini na moja hata baadhi ya majengo yake yako katika mtindo wa ujenzi wa zamani wa wakati wa Waarabu,Wajerumani na Waingereza hii imesaidia sana kuufanya mji kuwa katika hali ya kuvutia. Uongozi wa mkoa na jiji uliona badala ya kubadilisha majengo na kuruhusu watu kujenga majengo marefu hii ingefanya mji uwe na mandhari tofauti hivyo wao waliamua Jiji la Tanga la litabaki kama zamani Inaendelea uk. 2 Baadhi ya nyumba zitakazojengwa Pongwe City na kuuzwa. Redio za Tanga zaleta manufaa kwa wananchi Ziko sa kwa mkoa mzima

Upload: thechoice-tanzania

Post on 20-Oct-2015

676 views

Category:

Documents


7 download

DESCRIPTION

TOLEO LA 7

TRANSCRIPT

SAUTI YA TANGA

ISSN-1821-8946 TOLEO LA 7 - FEBRUARI, 24-1 MACHI, 2014 BEI. SH.500

Pembe Mills kuweka matangazo Mkwakwani

SAUTI YA TANGAUK.11

Coming together is a BeginningKeeping together is ProgressWorking together is Sucess CONTACTS: HEAD OFFICE: Whole sale & Retail Jamhuri St.Sub-Whole Sale: 14 Sikukuu Msimbazi St.BRANCH: Haidery Plaza / Ground Floor.ADDRESS: P.o. Box 20073, DSM - TEL: 2117090 / 2117358 FAX: 2117357 MOBILE: 0713 325488E-MAIL: [email protected]

For all your school and office requirement

PRIDE OF THE NATIONSIMBACEMENT

SIMBACEMENT

REGISTERED OFFICETanga Cement Company LimitedKorogwe Road, Pongwe Factory AreaP.o. Box 5053, Tanga TanzaniaTel: + 255 27 2644500 - 2/2610604Mob: + 255 784 644500Fax: + 255 272646148Website:www.simbacement.co.tz

DAR ES SALAAM OFFICE:3rd Floor, Coco Plaza, 254 Toure Drivep.o. Box 78478, Dar es Salaam, TanzaniaTel. + 255 22 2602778-9/2602784Mob: + 255 685 602784Fax: + 255 22 2602785Email: [email protected]

Pongwe City mji mpya wa Tanga

Ijue Pongwe City uk.3Uwanja wa Mkwakwani

uk.11Redio za Tanga uk.2

Na Wiliam Mngazija

KATIKA kile ambacho kinaonekana ya kuwa uongozi wa mkoa wa tanga na jiji hawataki kuharibu mandhari ya jiji

la Tanga wameamua ya kuwa ni vyema wajenge mji mpya ili kuacha mandhari ya jiji la Tanga ibaki kama ilivyo.

Kitendo hiki ambacho kimeafanywa na mkoa wa Tanga na uongozi wa jiji ni cha kupongezwa kwani mpaka hivi sasa mji wa Tanga ni kati ya miji ambayo inasifika kwa kuwa na mandhari yake halisi.Jiji la Tanga limepangika vizuri bado utakuta kuna mitaa ya kutoka barabara ya kwanza mpaka ya ishirini na moja hata baadhi ya majengo yake yako katika mtindo wa ujenzi wa zamani wa wakati wa Waarabu,Wajerumani na Waingereza hii imesaidia sana kuufanya mji kuwa katika hali ya kuvutia.

Uongozi wa mkoa na jiji uliona badala ya kubadilisha majengo na kuruhusu watu kujenga majengo marefu hii ingefanya mji uwe na mandhari tofauti hivyo wao waliamua

Jiji la Tanga la litabaki kama zamani

Inaendelea uk. 2Baadhi ya nyumba zitakazojengwa Pongwe City na kuuzwa.

Redio za Tanga zaleta manufaa kwa wananchiZiko tisa kwa mkoa mzima

SAUTI YA TANGA2 MATANGAZO

MAONI YA MHARIRI

BODI YA UHARIRIBODI YA UHARIRI

Mwenyekiti;Makamu Mwenyekiti ; Dessa Mamboleo MakokoMhariri Mkuu; William MngazijaMatangazo; Seif Ahmed Clement Mang’enya Damaris MahimboMasoko; Mariam MhinaBarua pepe: [email protected]: 0655-853650

KWANZA tunaomba samahani mwaka huu wa 2014 kwa kuchelewa kutoa toleo la Sauti ya Tanga kwa wakati una-ostahili sababu kubwa tulikuw tunafanya tathmini ya kip-indi cha nusu mwaka tangu tulipoanzisha gazeti hili mwezi wa Julai mwaka 2013 ili kujua je wasomaji wamelipokeaje

hii itatusaidia kujua tumefikia hatua gani.Tunashukuru ya kuwa gazeti letu wasomaji wamelipokea vizuri na

tumekuwa tunapokea simu kuulizwa vipi hili gazeti mbona mwezi huu hatujaliona mtaani sisi ni wajibu wetu kuchukua maoni na ushauri wa wasomaji wetu ili tuweze kuboresha gazeti hili.Katika baadhi ya mao-ni ambayo tuliyapata wengi wa wasomaji wetu walitushauri ya kuwa ili tuweze kwenda na wakati ni vizuri gazeti letu likasomwa kwenye mtandao “on line’’.Wao wanalalamika ya kuwa kila linapochapishwa huwa wakati mwengine wanachelewa kulipata kwa hiyo itakuwa vy-ema wakilisoma kwenye mtandao halikadhalika wasomaji wengine waliomba waongezewe makala mbali mbali kama vile hadithi,mambo ya utamaduni,afya,elimu na hata wengine waliomba ya kuwa litoke kila siku.

Tunasema kadri siku zinavyokwenda mawazo haya tunayakubali na yapo ambayo tunaaanza kuyafanyia kazi kwani kuanzia mwezi wa Machi tunategemea ya kuwa gazeti hili utaweza kulisoma kwenye mtandao na hivi sasa wakati bado linaandaliwa liko kwenye majaribio tafadhali fungua:Google:www.sautiyatangatz.blogspot.com .

Mtandao huu tutakuwa kila siku ana kila saa tunaningiza habari mpya za mkoa wa Tanga kwa maana hiyo wewe msomaji utakuwa na nafasi ya kuweza kupata habari za kila siku za mkoani Tanga pamoja na picha na tunakushauri kila siku uwe unalifungua matandao wako kuweza kujua kinachoendelea.Pia katika mtandao huu tutaweza kutoa mataoleo yote ya siku za nyumba ambayo bado ulikuwa huyasoma usikose fursa hii. Tutawasadia hata wale watangazaji wadogo wadogo wataweza kuweka matangazo yao katika mtandao kwa kwa bei nafuu lengo na sera ya gazeti letu ni kutangaza shughuli zetu za biashara za mkoa wetu ili tuweze kuvutia wawekezaji.

Katika toleo hili la jipya la mwaka huu pia tumeanzisha ukurasa maalum wa hadithi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu wa hadithi ipo hadithi murua ya kuuburudisha moyo wako ambayo iimetungwa na mtoto wa marehemu gwiji la utuzunzi wa hadithi hapa nchini ham-mie rajabu mtoto huyu nae katunga haidithi ijulikanyo kama “KIVUMBI CHA SAADANI” tafdhali usikose kuisoma maboresho mengine ya gazeti mliyotuletea yatafuata baadae. Naomba mtuvumilie maana mvumilivu hula mbivu asante.

KATIKA kile ambacho kinaonekana ya kuwa uongozi wa mkoa wa tanga na jiji hawataki kuharibu mandhari ya jiji la Tanga wameamua ya kuwa ni vyema wajenge mji mpya ili kuacha mandhari ya jiji la Tanga ibaki kama ilivyo.

Kitendo hiki ambacho kimeafanywa na mkoa wa Tanga na uongozi wa jiji ni cha kupongezwa kwani mpaka hivi sasa mji wa Tanga ni kati ya miji ambayo inasifika kwa kuwa na mandhari yake halisi.Jiji la Tanga limepangika vizuri bado utakuta kuna mitaa ya kutoka barabara ya kwanza mpaka ya ishirini na moja hata baadhi ya majengo yake yako katika mtindo wa ujenzi wa zamani wa wakati wa Waarabu,Wajerumani na Waingereza hii imesaidia sana kuufanya mji kuwa katika hali ya kuvutia.

Uongozi wa mkoa na jiji uliona badala ya kubadilisha majengo na kuruhusu watu

kujenga majengo marefu hii ingefanya mji uwe na mandhari tofauti hivyo wao waliamua watenge eneo jingine la jiji ili kujenga nyumba za kisasa.Mheshimiwa mstahiki Meya Guledi anasema jambo hili ni kuleta maendeleo bila ya kubadili mazingira ya awali ya mji.

Mji wa Pongwe City utasaidia sana kupunguza vurugu kati kati ya mji wa Tanga kwani umepangwa na utajengwa katika mtindo wa kisasa kwa kujitegemea wenyewe. Mji huu unatarajiwa yakuwa utakuwa na huduma zote muhimu kama maduka makubwa shopping malls,shule,hospitali,benki na hata baadhi ya ofisi zitakuwa huko.Hii itasaidia sana kupunguza muda wa kufauta huduma na mahitaji jijini.

Jiji nalo katika kuhakikisha ya kuwa mradi huu unafanikiwa hali kadhalika nao wameamua kuanzisha kituo kipya ch

mabasi ambacho kitajengwa eneo la Kange kwa maana hiyo hii pia itasaidia kupunguza wingi wa magari makubwa ambayoyanaingia mjini.

Mji huu umekaa mahalipazuri kwani ni kilomita 15 tu kutoka jijini Tanga hali kadhalika uko karibu na viwanda vikubwa vya siment kama Tanga cement na rhino Cement ambavyo viko umbali wa kiasi cha kilomita kati ya 3 na 6 na hata kwa wale ambao watapenda kusafiri kwa kutumia usafiri wa wa anga[ndege] ni kilomita 10 tu mpaka kufika kiwanjani.

Mradi huu ni mpango ambao unaendeshwa baina ya Jiji la Tanga na kampuni ya Amboni na kwa wale ambao watapenda kupata viwanja vya kujenga na kukodisha majengo wanaweza kuwasiliana nao kwa kutumia anuani 0767711120 na 022227772494 au kwa anuani ya mtandao:[email protected].

Na Mwandishi wetu

JIJI la Tanga hivi sasa limekuwa na mabadiliko ya haraka kutokna na kuwa redio unaweza jambo hili usilione kwa haraka lakini hebu chukua muda ukifika Tanga kufungua baadhi ya redio ambazo zinarusha hapa mjini ndyo utangungua kweli kuna mabadiliko.Tangu serikali iruhusu vituo bi-nafsi vya redio wananchi wamekuwa na uchaguzi mkubwa wa kusikiliza ladha tofauti za matangazo ya redio tangu zile za kijamii mpaka zile za dini.

Zipo redio ambazo ni kongwe na zamnai kama vile TBC,Redio One Sterio,Clouds nazo pia zina wapenzi wake lakini hizi zimekuwa zinarusha matangazo yake kutoka nje ya mkoa wa Tanga vi-tuo vikiwa ni Dar salaam.hivi sasa zipo redio zaidi ya saba ambazo hurusha matangazo yake kutoka hapa jijini Tanga kama vilePangani Fm

Akizungumza na gazeti gazeti hili mmoja wa watangazaji wa redio za jijini tanga Bwana Kas-simu Ali wa redio Ihsaan alisema inagawaje re-dio yao sera yake ni ya dini lakini matangazo yao yamewalenga wakazi wote wa mkoa Tanga na lengoni kukidhi haja ya kila jamii. Tangu waanze kutangaza matangazo hayo hawajawhi kupata matatizo yeyote kutoka kwa wasikilizaji kikubwa zaidi wanapokea kila mara pongezi.Alisisitiza za

kuwa hizi rdio za mikoa ni lazima zifuate maudhui ya wakazi wake wa eneo ambalo wanatangaza ili waweze kujua wanahitaji kitu gani bila kusahahu mila na tamaduni za eneo husika.

Mwandishi pia alipta fursa ya kuwasiliana na mtangazji wa redio Pangani FM bwana Mohamed Hammie maarufu kwa jina la uncle Mo ilikupata maoni yake hasa ukizingatia ya kuwa eneo ama-blo anafanya kazi ya kutangaza ni Wilaya ambayo inashika sana ustaarabu. Lakini naye alimhakik-ishia mwandishi ya kuwa “Kimsingi redio ya pangani FM imekubalika vizuri sana na kabla ya kuanza walifanya ufafiti ili kuona ni vionjo gani vitawafaa wakazi wa mameneo hayo.Kwa hivi sasa wanaongoz katika kupata wasikilizaji katika redio yao.

Tatizo kuwa ambalo linavikabili vituo hivi pamoja na kutoa huduma nzuri ni shida ya ma-tangazo bado mwako wa watu na makamupuni kutangaza biashara zao katika redio ni mdogo upo umuhimu wa kuwaelemisha wananchi kuhu-su umuhimu wa matangazo. Lakinini kwa upande wa wananchi kutuma kadi na kushiriki katika mijadla wengi hufanya hivyo na huwa hawajali kama redio hii hii ni ya dini gani huu ni ushiriki-ano mzuri ambao unatakiwa kuendelezwa na kila mtu.

SAUTI YA TANGA KUSOMWA KATIKA MTANDAO

Pongwe City mji mpya wa Tanga

Redio za Tanga zaleta manufaa kwa wananchiMajengo ya biashara ya Pongwe City.

Majengo ya ofisi za Pongwe City.

SAUTI YA TANGATANGAZO 3HABARIJumatatu Februari 17, 2014

11TANGAZOIjumaa Februari 14, 2014

10 TANGAZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wafanyabiashara kwa ujumla kuwa inasikitishwa na mgomo wa wafanyabiashara kwa kufunga maduka maeneo mbali mbali nchini.

Ifahamike kuwa matumizi ya mashine ya EFD ni jambo la kisheria na lilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010.

Pamoja na sheria kupitishwa, viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko kwa nyakati tofauti kwa kuanzia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Machi 2011.

Pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Billal alikazia jambo hili tarehe 8 Mwezi Novemba mwaka 2013.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alilitolea tamko pia Mwezi Desemba 2013 wakati akiahirisha Bunge kwa kusisitiza msimamo wa serikali kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi wa mashine za EFD.

Tarehe 29 Janauri 2014, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliweka bayana msimamo wa Serikali kwa kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni swala la kisheria na litaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa nyongeza kwa wafanyabiashara kununua mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014 baada ya kuongeza muda mara tatu kwa nyakati tofauti.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pia kwa nyakati tofauti

na maeneo tofauti imelitolea tamko jambo hili na itaendelea kufanya hivyo.

Kwa masuala ya kiutendaji yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo utoaji wa Elimu kwa umma.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inapenda kuwafahamisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa watu wanaolazimisha wafanyabiashara wenzao kufunga maduka kwa kuwatishia na kuwashurutisha wanavunja sheria kwa kusababisha uvunjifu wa amani nchini na hivyo mkono wa sheria utawafikia. Pia imefahamika kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa bali hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya.

TRA imekuwa ikipokea taarifa na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara na wananchi wema wakiomba ulinzi ili wafungue maduka yao na kufanya biashara maana ndio ajira yao na mahali pakujipatia riziki ya kila siku.

Ifahamike kwamba wale wote wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja sheria kwa kuwalazimisha wafanyabiashara kugomea agizo halali la kisheria hivyo kwa wale wote wanaotishiwa au kushurutishwa watoe taarifa kwa kupiga simu namba zifuatazo 0786 800 000, 0713 800333, 0800 110016 au barua pepe [email protected] au kituo cha polisi kilicho karibu.

“PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”

IMETOLEWA NA KAIMU KAMISHNA MKUUMAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

ISO 9001: 2008 CERTIFIED

!

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wafanyabiashara kwa ujumla kuwa inasikitishwa na mgomo wa wafanyabiashara kwa kufunga maduka maeneo mbali mbali nchini.

Ifahamike kuwa matumizi ya mashine ya EFDs ni jambo la kisheria na lilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010.

Pamoja na sheria kupitishwa, viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko kwa nyakati tofauti kwa kuanzia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Machi 2011.

Pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib Billal alikazia jambo hili tarehe 8 Mwezi Novemba mwaka 2013.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda alilitolea tamko pia Mwezi Desemba 2013 wakati akiahirisha Bunge kwa kusisitiza msimamo wa serikali kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi wa mashine za EFD.

Tarehe 29 Janauri 2014, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliweka bayana msimamo wa Serikali kwa kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni swala la kisheria na litaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa nyongeza kwa wafanyabishara kununua mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014 baada ya kuongeza muda mara tatu kwa nyakati tofuati.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pia kwa nyakati tofauti na maeneo tofuati imelitolea tamko jambo hili na itaendelea kufanya hivyo.

Kwa masuala ya kiutendaji yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo utoaji wa Elimu kwa umma.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inapenda kuwafahamisha wafanyabiashara na umma kwa ujumla kuwa watu wanaolazimisha wafanyabishara wenzao kufunga maduka kwa kuwatishia na kuwashurutisha wanavunja sheria kwa kusababisha uvunjifu wa amani nchini na hivyo mkono wa sheria utawafikia. Pia imefahamika kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa bali hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya

TRA imekuwa ikipokea taarifa na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wema wakiomba ulinzi ili wafungue maduka yao na kufanya biashara maana ndio ajira yao na mahali pakujipatia riziki ya kila siku.

Aidha ifahamike kwamba wale wote wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja sheria kwa kuwalazimisha wafanyabiashara kugomea agizo halali la kisheria hivyo kwa wale wote wanaotishiwa au kushurutishwa watoe taarifa kwa kupiga simu namba zifuatazo 0786 800 000, 0713 800333, 0800 110016 au barua pepe [email protected] au kituo cha polisi kilicho karibu.

“PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”

IMETOLEWA NA KAIMU KAMISHNA MKUUMAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

SAUTI YA TANGA4 MAKALA

Na Damarisi John Mahimbo

1.VICHAA WA TANGAMnisamehe katika kutumia neon la vichaa lakini lengo langu ni kufikisha ujumbe huu kwa wahusika. Pengine ni vizuri tuawite watu hawa ni wagonjwa wa akili. Hapa jijini Tanga wa aina hii ni wengi sana na takwimu zaonyesha ya kuwa idadi yao ni kubwa ku-liko idadi ya magari yaliyopo hapo jijini. Kwa ushauri wangu nadhani upo umuhimu wa idara ya Usatawi wa jamii kufanya zoe-zi la kuwakusanya na kuwaweka sehemu inayostahili hasa ukizingatia ya kuwa jiji linatarajiwa kuwa nwageni wengi ambao ni wawekezaji hali kama hii ni tishio kwa wageni na hata wananchi.Nilijaribu kuuliza watu wengi na hasa wazee tatizo la hawa watu kuwa wengi ni nini wakasema wengi wao wamerogwa kutokana na matatizo mbali yakiwemo ya wizi.

2. VYOO VYA KULIPIA TATIZOUkiwa mjini Tanga ni tatizo kubwa sana

kujisaidia kwani ukitembelea maeneo hayo unaweza kupata shida ya kujisaidia hii ni kwa sababu ya uhaba wa vyoo vya kulipia.Eneo hili ambalo tunaliita ni kati kati ya mji kipo choo ambacho kilijengwa na Mjeruma-ni lakini cha kushangaza hakitumiki na watu wanajisaidia nje.Hali kadhalika barabara ya Jamaa napo kipo choo kimepigwa rangi na kubandikwa tangazo la Salama Condom la-kini milango imefungwa kwa kupigwa ma-bati.Haya hebu fikiria kama umeshikwa na haja unajisaidiaje nashauri Jiji lingetangaza tenda ili kama wapo watu ambao wanapen-da kuendesha vyoo hivyo na kulipa ushuru mdogo kwa jiji waruhusiwe.Hebu wazee wa Jiji lioneni hili.

3. MAKABURI YA WAJERUMANI NA

TANGA KUNANI?

KIFUA KISICHO NA KICHWAHebu pita pale kwenye makaburi ya wa-

jerumani ambayo yanatazamana na ofisi za CRDB katika moja ya kaburi juu yake utaona kifua cha umbo la mtu ambacho hakina kichwa …..lakini pia kimepakwa rangi nyekundu kama vile kinavuja damu na hakina kichwa.Nashindwa kuelewa ile sanamu ya udongo ilikuwa ni ya Mzungu wa mkongeni au Mwafrika aliyefanya kazi katika serikali ya mkoloni.Pengine hawa watu wa URITHI wangeweza kwenda ku-kichukua na kukihifadhi huku wakifanya utafiti ni cha nani na kusema kweli ki-mechongwa vizuri katika nchi za wenzetu huko Ulaya hii ni kumbukumbu muhimu sana.Kazi kwenu URITHI

4 SAKARANI AKUMBUKWA MAKABURI YASAFISHWA

Napenda sana kuwapongeza uongozi wa Jiji kwa kufanya usafi katika eneo la maka-buri ya askari wetu ambao walipigana ka-tika vita vya kutetea mji wa Tanga miaka 100 iliyopita. Katika toleo letu la sita mwezi wa Disemba mwaka wa jana tulitoa taarifa ya kuwa eneo hilo limegeuka kuwa choo kwa sababu ya majani ambayo yalikuwa yameota na hakuna anaeyakata. Pengine sasa ni vizuri jiji likatoa nafasi ili watu am-bao wanapenda kufanya eneo hilo liwe la

utalii wapewe nafasi hiyo ili walioboreshe na walipe ada kwa jiji la Tanga.

5. SAA IPI YASEMA KWELI YA RAHALEO AU YA STENDI?

Pale ofisi za Raha ya Leo mjini Tanga wakati umekaa katika viti ukisubiri upande basi ndipo utaona maajabu ya saa kwa sababu wana saa inakwenda kwa wakati wake lakini na ile saa ya stendi iliyopo pale sehemu ambayo polisi wa Trafiki wanasi-mama nayo inaenda vyake.Kusema kweli huwezi kujua saa ipi ina sema ukweli kwani kuna siku nilifuata ile ya stendi nikasema niiingie sokoni Ngamiani nikatafute mboga [Papa] kuja kurudi basi limeondoka.Ku-wauliza wanasema nikiwa pale Raha leo ni-fuate saa yao sijui inakwenda kwa kufuata masaa ya Afrika ya Mashariki au Afrika ya Kati sijui.Kuuliza nauli nikaambiwa imeku-la kwangu nimechelewa mwenyewe gari kwa kutafuta papa.Haya ingekuwa wewe yamekukuta ungeanzia wapi?

6. OFISI YA MENEJA CRDBUkifika katika benki ya CRDB Tanga

pana kichekesho.Lipo tangazo linaonye-sha ya kuwa hapa ni Ofisi ya Meneja la-kini cha kuchekesha ni kuwa tangazo hilo limewekwa juu ya dirisha sasa sijui unapi-tia dirishani kwenda kumwona Meneja? Ukichungulia zaidi utaona kwenye lile di-

risha ni nje uani mmmh….. mengine uki-yaona wayaacha nadhani hili wataliona na kulirekebisha.

7.BAISKELI ZA RAHA LEOUkifika pale Raha Leo kama wewe um-

safiri na unataka kwenda chooni kujisadia ukienda huku uwani utakuta baiskeli yingi na zote zimefanana.Mara ya kwanza nilid-hani ni mizigo ya baiskeli inasafirishwa kwenda Dar es salaam lakini nilikuwa nao-na kila siku haipungui.Ikabidi nifanye ki-jiutafiti cha kimya kimya ndio nikangundua ya kuwa kumbe kila mfanyakazi pale Raha Leo pale ofisi ya Tanga tangu wale mais-npekta wa magari,wakata tiketi,wapakia mizigo,madereva,makondakta kila mtu ana baiskeli.Sasa sijui wale walioko ofisi ya Dsm wao wanatumia nini kwa sababu wakipewa baiskeli au piki piki kutokana na trafiki ya mjini ni majanga…….lakini wale wa ofisi ya Dodoma wanaweza wakapewa punda sijui wenyewe Raha Leo wanasema-je maana ni ushauri tu!

8. UKARABATI WA NYUMBA ZA POLISI CHUMBAGENI

Hebu pita pale kwenye nyumba za polisi wa chumbageni utaona huo ukarabati wal-ioufanya kwenye nyuba ni babu kubwa.Sijui walitumia mkandarasi gani kwani wa-mechukua mabao na kugeuza sehemu ya mbele ambayo ni veranda kuwa vyumba.Sasa wajiuliza kibali cha ukarabati walipa-ta wapi na je wao ndio washika sheria nani ataweza kumfunga paka kengele lakini hii nakushauri utazame kwa mabli usisogee na kujitia kupiga picha kwani unaweza kuishia mikononi mwao.We fanya kama unatembe-lea kwa pembeni simama upande wa Tanga Hotel ila usisogee karibu utalianzisha jipya utakaloshindwa kulimaliza

Na Sechuma Nkuninga

TANGU zama za ukoloni kilimo cha mkonge kilikuwa ni cha mashamba makubwa yaliyoku-wa yakimilikiwa na wakulima wakubwa wa kikoloni.Mnamo

mwaka 1967 serikali ilitaifisha sehemu kubwa ya mashamba hayo na kuanzisha shirika la mkonge Tanzania (TSC) lil-ilopewa jukumu la kumiliki mashamba hayo.Mwaka 1973 mamlaka ya mkonge Tanzania (TSA) ilianzishwa ili kumliki na kusimamia uendelezaji wa zao la mkonge.

Katika kutelekeza sera mpya za ma-geuzi ya kiuchumi ya soko huria mwaka 1985 serikali ilibinafsisha mashamba kwa sekta binafsi.Kufikia mwaka 2005 serikali kupitia Tume ya Raisi ya kureke-bisha mfumo wa mashirika ya umma (PSRC) ilikamimisha ubinafsishaji wa mashamba yaliyokuwa chini ya mamla-ka ya mkonge Tanzania.kwa kuwa sekta ya mkonge inaendeshwa kwa asilimia mia moja na sekta binafsi hivyo serikali kupitia bunge lake mwaka 1967 iliunda Bodi ya Mkonge kwa ajili ya usimamizi wa sera,udhbiti wa ubora,masoko na utafiti wa masuala yote yanayohusu zao la mkonge nchini.

Kilimo cha mkonge nchini kina his-toria ndefu ya zaidi ya ya karne moja tangu zao la mkonge kuingizwa nchini mwaka 1893.Tangu zama za ukoloni na hata baada ya uhuru wa Tanganyika na sasa Tanzania kilimo cha zao hili kime-kuwa kikiendeshwa zaidi na wakulima wakubwa[plantation estates].katika zama hizi ambapo mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sehemu kubwa ya nchi yetu.Bodi ya mkonge Tanzania ime-azimia kuhamasisha kilimo cha zao la

Mkonge utaleta mapinduzi nchini

mkonge kwa wakulima wadogo ambao kimsingi ndio waathirika wakuu wa ma-badiliko ya tabia nchi.

Sera hii kimsingi ilianza kutekelezwa tangu miaka ya 1960 ambapo mfumo wa kwanza wa kilimo cha wakulima wado-go wa mkonge ulianzishwa katika eneo la Kabuku katika wilaya ya Handeni. Hata hivyo mfumo huu haukudumu kwa muda mrafu na hatimaye ulikufa kuto-kana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni wananchi kutoanadaliwa na kushirik-ishwa kikamilifu kulima mkonge kupitia mfumo huu.

Baada ya muda mrafu kupita wa kili-mo cha mkonge kwa wakulima wadogo ulianzishwa tena rasmi mwaka 1999 na kampuni ya Katani Ltd. Mbali ya wakuli-ma wadogo walio chini ya mfumo una-osimamiwa na kampuni ya katani,pia kuna wakulima wadogo kwenye maeneo mbali mbali ya mkoa wa Tanga na kanda ya Ziwa ambao wameamua kujiingiza ka-tika kilimo cha mkonge katika masham-ba yao binafsi baada ya kuhamasishwa na bodi ya mkonge Tanzania. Kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya wakulima wadogo wa zao la mkonge 5,000 wanaji-

husisha na kilimo hiki katika mikoa ya Tanga,Mara,Shinyanga na Mwanza.

Kutokana na mabadiliko makubwa ya tabia nchi kwa sasa wakulima am-bao wengi wao ni wakulima wadogo wamekuwa wakikosa mavuno kutokana na kutegemea mvua ambazo kwa sasa mtiririko wake sio mzuri hivyo kupoteza matumaini kwa wakulima walio wengi.Je Bodi ya Katani imefanya nini kulikabili tatizo hilo soma mwendelezo wa habari hii katika toleo lijalo na baadae tutkue-lezea vizuri shughuli za kampuni ya ka-tani Limited.

Mkonge ukiwa shambani Hale

Hebu pita pale kwenye makaburi ya wajerumani ambayo yanatazamana na ofisi za CRDB katika moja ya kaburi juu yake utaona kifua cha umbo la mtu ambacho hakina kichwa …..lakini pia kimepakwa rangi nyekundu kama vile kinavuja damu na hakina kichwa.Nashindwa kuelewa ile sanamu ya udongo ilikuwa ni ya Mzungu wa mkongeni au Mwafrika aliyefanya kazi ka-tika serikali ya mkoloni.Pengine hawa watu wa URITHI wangeweza kwenda kukichukua na kukihifadhi huku wakifanya utafiti ni cha nani na kusema kweli kimechongwa vizuri katika nchi za wenzetu huko Ulaya hii ni kumbu-kumbu muhimu sana. Kazi kwenu URITHI

SAUTI YA TANGA 5MAKALA MAKALA

Na Aisha Msofe, Pangani

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya

Pangani Bibi Zabibu Shaaban amewataka vijana wilayani Pangani kuiga mfano wa vijana wa kijiji cha MSEKO ambao wameamua na kujikusanya ili kuunda vikundi ambavyo vimeelekeza nguvu zao katika suala la kilimo.

Hayo ameyasema wakati alipotembelea katika kijiji cha Mseko kwa ajili ya kukagua eneo la shamba lenye ukubwa wa ekari mia moja lililolimwa na kutengwa kwa ajili ya vijana wa kijiji hicho ili wajishughulishe na shughuli za kilimo.

“Nahamasisha vijana ili wajiunge kwenye vikundi vya ufugaji nyuki, vikundi vya ukulima pamoja na vikundi vingine ambavyo vinaonekana ni vya manufaa ili vijana waweze kunufaika kwa pamoja.Zoezi hili litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana”. Alisema Bi Zabibu.

Kwa upande mwengine pia Bi Zabibu amewataka vijana wilayani Pangani wajikusanye na kuunda vikundi ambavyo wataweza kubuni miradi mbalimbali ili kuirahisishia serikali kutoa msaada kwa vikundi.

Nae mwenyekiti wa kamati ya mazingira kijiji cha Mseko Bwana Sadi Mgoda amesema ya kuwa, vijana kijiji hicho wamefurahi na wanaushukuru sana uongozi wa wilaya kupitia idara ya misitu na kitengo cha nyuki kwa kuwapatia msaada wa vifaa vya ufugaji nyuki kwa ajili ya kuboresha shughuli zao.

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA KUTAFUTA MATANGAZO

Waraka kutoka PanganiVijana Mseko waunda kikundi cha ujasiriamaliMkurugenzi Mtendaji awapongeza

Sauti ya Tanga inapenda kuwatangazia ya ku-wainahitaji watafutaji wa matangazo kwa ajili

ya gazeti lake. UTALIPWA KAMISHENI 20%

Wasiliana nasi kwa simu 0655-853650au Barua pepe:[email protected]

Na Aisha Msofe, Pangani

UKARABATI wa mabweni ya shule ya sekondari ya Bushiri iliyopo kijiji cha Msaraza bado haujakamilika na umetajwa ya kuwa ndio sababu ya kutowekwa kwa jiwe la msingi ili kuruhusu kutumika kwa mabweni hayo.

Akizungumza na gazeti hili mkuu wa wilaya ya Pangani Mheshimiwa Hasfa Mtasiwa amesema ya kuwa, mbali na kutokamilika kwa ukarabati huo, shule hiyo pia inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji hali inayomfanya kutofungua mabweni hayo. Haya ni makubaliano waliyoafikiana na Naibu Waziri wa Tamisemi Mheshimiwa Aggrrey Mwanri wakati wa ziara yake mwaka wa jana.

“Mabweni yale tulikuwa tunatarajia tuyazindue mwka wa jana lakini kikwazo kikubwa ni kuwa bado hakuna maji. Ila tumepata wafadhili na mwaka huu tutawafutilia kwa karibu ili kutusaidia suala hilo” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mabweni hayo yalitakiwa yafunguliwe na Naibu Waziri wa Tamisemi Mheshimiwa Aggrrey Mwanri mwezi wa nane mwaka wa jana wakati wa ziara yake wilayani Pangani, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kubaini ya kuwa yamejengwa chini ya kiwango na hivyo kumuomba Mkuu wa Wilaya afungue majengo hayo kwa niaba yake.

MABWENI YA SEKONDARI

BUSHIRI HAYAJAKAMILIKA

Mtalii akiwa baharini Pangani

SAUTI YA TANGA 6MATANGAZO

RATCO EXPRESS BUS SERVICEKwa usafiri salama na wa uhakika

i

SAUTI YA TANGA 7

TANGA BEACH RESORT

Eliminate travel stress by staying at a convenient hotel in Tanga boasting easy access to major tourist attractions in Tanga Region including Saadani National Park, Amboni Caves, Amani Nature and the exotic Indian Ocean.

From Tanga Beach Resort, you can travel down to Pangan iCoast, a historical site which serve as a reminder of the strong Arabic and later German, British colonial period in East Africa. You will enjoy and experience nature, history, culture and beach relaxation.

OTHER SERVICES AVAILABLE FROM US IS: • Meetings / Conferences in fully furnished and equipped with modern facilities. • Live Music and orchestra from some of the best local and international bands during special occasions and summer holidays.

• WEDDINGS / ANNIVERSARIESYou can celebrate your event at our hotel and enjoy delicious food, music and serenity!

• SEA ADVENTURE The hotel offers routine trips adventure. If you are interested justlet us know in advance.

• CUSTOM TAILORED EVENTS You can host your private event at our hotel. Just tell us your idea/ requirements and we will do therest.

Tanga Beach Resort is not only the best

luxury hotel in Tanga, it is also the

best luxurious hotel for tourists and

business travellers in Tanga, Tanzania.

It started operations in the year 2009.

The Hotel is located adjacent to the

In¬dian Ocean in Tanga city which

has a dynamic and historic past.

HOTEL MOBILE:+255-785171717+255-683750000/850003EMAIL: [email protected]: www.tangabeachresort.com

ENJOY A TRUE HOLIDAY EXPERIENCE

P.O. BOX. 2294, TANGASIMU: +255-272645424/5FAX: + 255272645426

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

KUHAMA KWA OFISI ZA MAKAO MAKUU

YA SHIRIKA

Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kuwa Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa zimehamia kwenye Jengo lake jipya lililopo Kiwanja Na. 1 kwenye makutano ya Barabara za Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, eneo la Upanga jijini Dar es Salaam.

Aidha tunapenda kuwaomba wateja wetu wa Dar es Salaam kwamba wakati Shirika likiendelea kukamilisha zoezi la kuhamisha ofisi zake waendelee kupata huduma katika ofisi za Mikoa ya Shirika za Ilala, Temeke, Kinondoni na Upanga.

Utaratibu wa kuhamisha Makao Makuu ya Shirika unafuatia maboresho mbalimbali yanayofanywa na Shirika tangu mwaka 2010 kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano 2010/15 unaolenga kuboresha huduma kwa wateja na wananchi kwa ujumla.

SAUTI YA TANGA8 HADITHI / MAKALA

NILISTUSHWA na breki za ghafla zilizofungwa na dereva aliyekuwa tayari keshapata ari ya kunyonga usukani, na kukanyaga

mafuta kwa safari ndefu.Kama si kuunyosha mkono wa kulia na

kujizuia, paji la uso wangu lingekwenda moja kwa moja kugonga kwenye siti iliyokuwa mbele yangu.

Nilijizuia kwa nguvu mpaka gari iliposimama kwa mwendo wa kunyata, ndipo nilipoutoa mkono wangu na kujiweka sawa pale nilipokuwa nimekaa.

Sikuwa na haja ya kuuliza sababu ya gari kusimama, kwani kwa mbali sana tayari nilimsikia kiongozi wa msafara Bwana Saidi Mapondanga akitangaza kusahaulika kwa mtu mmoja ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ni lazima mtu huyo asubiriwe kutokana tayari alishatoa gharama zake kwa ajili ya hii safari.

Kwa bahati mbaya wakati akitangaza, mimi nilikuwa kwenye nusu ya usingizi. Lakini nilipoamka tu kutokana na zile breki, niliweza kusikia baadhi ya abiria niliokuwa nao mle garini wakinong’ona kuhusiana na jambo hilo, hata hivyo sikumuuliza mtu. Nikabaki nasikiliza ile minong’ongo tu. Nukta chache baadae nikajua nini kinaendelea kwa wakati ule.

Nilisikia pia baadhi ya abiria wakilalama juu ya gari kusimama, wakidai kuwa huyo mtu aliyesahaulika ni uzembe wake mwenyewe na hivyo safari ingeendelea tu na ikibidi arudishiwe hizo gharama zake kwani bado tuna mwendo mrefu hadi tufike tulipopakusudia.

Hoja hiyo nilisikia ikiungwa mkono na watu wachache mle garini, lakini karibu nusu na robo ya abiria wote mle ndani niliowaona wakiwa kimya na kuendelea na masuala mengine, jambo lililopolekea hoja hiyo kufa kimya kimya.

Nilijitikisa kidogo pale nilipokuwa nimekaa, nikajinyoosha ili mwili upate kuwa sawa- kisha nikanyoosha mikono yote miwili juu taratibu kama nataka kujifyatua na kuirejesha chini kwa haraka.

Katika safari zote ambazo nasafiri huwa ni lazima nilale njiani. Hii inatokana na usiku wa kuamkia siku ya safari kutazama filamu, ama tamthilia kwa ajili ya kupunguza makali ya urefu wa safari ninayokwenda. Kulala njiani huwa kunanipunguzia uchovu, ndivyo nilivyo!!

Niligeuka kumtazama jirani yangu niliyekaa nae pale, macho yake na yangu yakagonga, kisha kila mmoja akayaondosha macho yake kwa haraka bila kusema neon.

Alikuwa ni mtu ni mzima wa makamo, kwa kumtazama haraka haraka unaweza kukadiria umri wake kati ya miaka 45 hadi 50. Alikuwa yupo ‘very smart’ na muonekano wa ukakamavu.

Mara nikamuona anatoa boksi la biskuti na kisha akachomoa biskuti mbili na kuanza kula. Nikamkata jicho mara moja kisha nitakazama pembeni, alipoona nimefanya hivyo, akalisogeza lile boksi la biskuti karibu yangu akiwa

na lengo nijichukulie, haikuwa hivi. Alikutana na kisiki.

Sio kwamba sipendi hiki chakula, la hasha!! Ila nikila huwa nakaukwa na mate kabisa, hasa eneo la koo. Nikila sharti soda ama maji yawe karibu. Nilimwambia asante na akawa mwerevu.

Papo hapo niligeuka tena kutazama upande wa pili. Nilikaa upande wa dirisha. Kwa haraka nikanyanyua mkono na kukinga macho yangu kukwepa mwanga wa jua uliokuwa ukipenya pale dirishani.

Sina matatizo ya macho,!! bali ndio kwanza nilikuwa natoka kusinzia, hivyo macho bado hayakuwa yamezowea mwanga. Kichwa kingeneuma endapo ningelazimisha kulikodolea macho lile jua.

Nikawa naibia kutazama mandhari ya nje kwa kufunua kidole kimoja baada ya kingine hadi macho yalipozoea ule mwanga, na kisha nikautoa mkono wote, sasa nikawa natazama vizuri.

Hakuna kilichonivutia pamoja na kupoteza dakika nzima kutazama nje. Nikashika kioo na kukifungua chote, walau upepo ukawa unapita mle garini, hasa upande niliokaa mimi. Yule niliyekaa nae pale akanigusa bega na kunionyeshea ishara ya dole gumba, ishara ya kufurahia ule upepo uliokuwa unaingia.

Nikampa tabasamu dogo kisha nikajiinua kidogo pale na kutoa kichwa nje. Nilitazama huku na huko. Mara! nikaona watu wanashuka, nikahisi itachukua muda mrefu kumsubiri mtu tuliyeambiwa tumsubiri.

Kwa namna moja ama nyengine niliwaza kwamba hili tulilokuwa tumeambiwa tufanye, ni kama upuuzi kwani waandaji wa safari walishatoa muda maalumu wa kukutana kwa pamoja ili sote tupate kuwa kwenye msafara mmoja...iweje basi huyu mtu mmoja achelewe!!??

Yeye ni nani hasa..!!?? Nilijiuliza swali hili kama mara tatu mfululizo, nilimgeukia Yule baba wa makamo aliyekuwa karibu yangu kutaka kumshirikisha Swali hili lakini ghala nikaghairi.

‘Ya Mungu Mengi!!’ nilijisemea kimoyoyo

Nilipoona kila mtu anataremka, na mimi nikafuata mkumbo baada kuona yule jirani yangu nae akifanya hivyo.

Dakika tano baadae gari zima likawa tupu. Wote tulikuwa nje tukipiga domo huku wengine wakijaribu kutafuta baadhi ya mahitaji.

Sikuwa nahitaji kitu, baada kuona nina salio la kutosha kwenye simu yangu. Hivyo nilikwenda moja kwa moja kujiegemeza kwenye mti wa mwembe uliokuwa hatua chache kutoka pale barabarani, karibu kabisa na liliposimama gari.

Eneo lote lilionekana kuwa na mandhari ya kijiji. Kwa kuwa ilikuwa ni asubuhi, palikuwa na akina mama wachache ambao walikuwa wakiuza vitafunwa pamoja na kijana mmoja aliyekuwa akikaanga mihogo.

Hapakuwa na fujo sana, labda nadhani ni kutokana na kuwa mapema mno. Mbele ya ule mti niliokuwa nimejiegemeza palikuwa na maembe yaliyoanguka hovyo, ila mengi yalikuwa yamekwishaoza.

Napenda sana maenbe, ila haya yalinitia kinyaa. Sikutaka kujua kwanini watu wa hapa wanayasaliti haya maembe hadi kufikia hali ile, kama wameyakinai kutoka na kuwa msimu wake, basi wangeyakusanya na kufanya biashara. Bado watanzania hatujafikia utajiri wa kutupa matumba kiasi kile, tena embe! Niliyatazama kwa masikitiko.

Wakati nataka kuwaza ni namna gani mtu tuliyekuwa tunamsubiri atatufikia pale, na ndio wakati huo kiongozi wa msafara Saidi Maponganda aliposimama na kutupasha habari kuwa kuna gari ndogo aina ya Cheser inamleta mtu huyo na hivi anavyozungumza yupo njiani analetwa.

“Naomba muwe na subira ndugu zangu, safari itaendelea punde tu huyu mtu atakapokuwa amefika, si mnafahamu umuhimu wa safari hii” ilikuwa ni sauti ya Bwana Mapondanga, sauti yake ilikuwa kavu na yenye mashaka.

Ajabu ni kwamba hakuna mtu eliyepingana na ile kauli, watu wote tulikuwa wasikivu!! Hapo ndipo niligundua kuwa wote tulikuwa tukitokea pwani, kwani ndio utaratibu wetu. Ustaarabu kwetu ni jambo la kawaida.

**************************Eneo tulilokuwa tumesimama

panaitwa Neema, moja ya kijiji kinachopatikana hapa mkoani Tanga; takribani kilometa kadha kutokea Tanga mjini kwa njia ya kuelekea Pangani.

Pangani ni moja kati ya wilaya nane zinazopatikana mkoani Tanga, ipo wilaya ya Kilindi, wilaya ya Handeni, wilaya ya Muheza, wilaya ya Tanga mjini, wilaya ya Mkinga, wilaya ya Lushoto pamoja na wilaya ya Korogwe.

Katika historia Pangani inapewa heshima kubwa hadi sasa. Watumwa wengi walikuwa wakitokea Pangani na kupelekwa Zanzibar. Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu.

Unaambiwa mwanzo wa ukoloni, Pangani ilikuwa mahali palipoanzia vita vya Abushiri mnamo mwaka 1889 dhidi ya utawala wa Wajerumani.

Baada ya kukomeshwa kwa vita hiyo, mji wa Pangani ulipungua sana kimaendeleo kwa sababu Wajerumani walikazia maendeleo ya mji wa Tanga.

Vita vya Abushiri vilikuwa jaribio la wenyeji wa pwani ya Tanganyika kuzuia utawala wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki mnamo mwaka 1888 hadi mwaka 1889, jaribio lililokandamizwa na jeshi la Wajerumani. Wajerumani waliita vita hii “Uasi wa Waarabu”.

Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya

Kivumbi cha Saadani!

Pangani, tena alikuwa mfanyabiashara mkubwa katika mji huo.

Tarehe 16 Desemba 1889 kiongozi huyo alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani.

Kwa kukadiria umbali wa kutoka Tanga hadi Pangani ni kilometa arobaini na saba. Lengo lilikuwa ni kupita hapo ili tuifikie mbuga ya Saadani kujionea wanyama pori ili kudumisha utalii wetu wa ndani. Nani kasema mtalii ni Mzungu peke yake. Tuna haja ya kujua maliasili zetu ili tupate kujivunia.

Kama nitafanikisha hili, basi itakuwa ni mara yangu ya kwanza kuona wanyama kama Tembo, Swala, Simba, Nyati, Twiga na Nyumbu ambao kwa siku zote za maisha yangu hadi kufikia leo nilikuwa nikiwaona kwenye runinga.

Kwa zile kilometa kadhaa ambazo tumezikata hadi kukifikia kijiji hichi cha Neema, nikajua bado tuna msafara mrefu sana wa kumaliza kwani sasa itatupasa tupite njia panda ya Mgwisha- hiki ni kijiji cha pili kutoka hapa.

Baada ya hapo tupite kijiji cha Maere, kisha Tongoni mahala ambapo yanapatikana magofu ya kale yaliyotokana na msikiti ambao waumini wa dini ya Kiislamu kutokea Persia walifika hapo na kusali. Persia ndio Iran ya leo.

Unaambiwa tangu karne ya 15 magofu haya yaliaminika kuwepo, na baharia kutokea nchini Ureno Vasco Da Gama aliwahi kufika eneo hilo na kukaa kwa siku 15.

Tukipita Tongoni dereva itamlazimu akanyage mafuta mpaka kijiji cha Geza, halafu ndipo tuingie Kirare na baadae kijiji cha Tundaua na Jiweni.

Kutokana na ramani tuliyonayo Gawani, Jitengeni na Ujenzi ni vijiji ambavyo tunapaswa kuvipita ili tupate kufika Kigombe kwa ajili ya “kuchimba dawa” na kupoza kiu.

Waliosema safari ni hatua hawakukosea, kwani pamoja na ukaribu wa kijiji cha Bago na Kimang’a lakini pia hatuwezi kufika Boza mahala panapopatikana njia ya kuelekea Muheza mpaka tupite Choba.

Kilometa sita kutokea Boza ndipo tutaingia Pangani mjini na baadae kuelekea kivukoni kwa ajili ya kuvuka ng’ambo ya pili na kuendelea na safari.

Ilikuwa yapata saa tatu na nusu asubuhi. Tayari dakika 15 zimeshapita tangu tuambiwe tuwe wavumilivu wa kumsubiri mtu aliyekuwa amesahaulika kwenye hii safari.

Pale tulipokuwa tumesimama kila mtu alikuwa ameshaondokewa na hali ya ugeni na woga kwa mwenzake. Tulijikuta tukizoeana ghafla!!!

Mtunzi: Mohammed Hammie (Anko Mo)

Phone: 0719000010E-mail: [email protected]

Itaendelea toleo lijalo

SAUTI YA TANGA 9MATANGAZO

Our branch is located along market street opposite Khanbhai pharmacy and very close to “soko la uzunguni”.

Tanga Branch- Box 1180, TangaTel: 027-2644353/2647763/2646875

Fax 027-2644270

SAUTI YA TANGA MAKALA10

Na Mariam Mnyamamkali

MKOA wa tanga un-aingia katika sera ya uwekezaji na ni dha-hiri lengo hilo litafai-kiwa kutokna na juhudi

ambazo zinzfanywa na mkoa katika kuhamasisha uwekeazji.Ndio saba-bu kila mara mkoa unajitahidi sana kuandaa maonyesho mbali mbali ili kuweza kuhamashisha wawekezaji. Suala la uwekezaji nalo linahitaji ku-tangazwa ndiyo sababu na sisis katika mchango wetu tuliamua kuanzisha gazeti la sauti ya Tanga lenye sera ya

kibiashara ili kutangaza shughuli za biashara na viwanda vyetu vya mkoa wa Tanga. Katika kufanikisha shughu-li hii tunatarajia kuandaa toleo maal-um la kutangaza shughuli za mkoa wa Tanga mwezi wa Julai (Special Sup-plement).

Tunategemea kabala ya kuandaa toleo hili tukutane na viongozi wa mkoa pamoja na wataalamu wa fani wa sekta mbali mbali kama vile kilimo,biashara,viwanda,elimu,uvuvi ili kuweza kupata mawazo yao.hali kadhalika tunategema kuandaa tanga Bussiness Directory ambayo itakuwa na orodha ya makampuni na viwanda

vyote na kuiweka katika mtandao wetu ili iwe rahisi mwekezaji kuweza kupata picha halisi ya shughuli za mkoa wa Tanga.

Hapa sasa ndio unakuja umuhimu wa kutangaza biashara tatizo kubwa ni kwamba makampuni mengi ya mkoa wa Tanga yamezoe kufanya biashara kwa uzoefu kwa kuwa ni makampuni ya zamnai kitu amba-cho kwa hivi sasa sio sawa kwani ushindani ni mkubwa sana.

Chukulia mfano wenye magazri wale wa zamnai hapa mjini Tanga ha-waoni kabisa umuhimu wa kutangaza biashara zao wao wanafikria kwa

kuwa jina linatambulika basi wateja wataendelea kusafiri kwa kutumia jina hilo hali kadhalika viko viwanda vya vinywaji baridi vya zamani na wao pia hawatangazji bidhaa zao sasa hata kama yupo mwekezaji anataka kujiunga nao au kuboresha kiwanda cha aanashindwa. Hili ndio tatizo kubwa linalotukabili na ni muhimu sana makampuni yetu ya mkoa wa Tanga yabadilike.Ni lazima waone umuhimu wa kutangaza bidhaa zao katika redio zetu za mkoa wa Tanga au kwenye gazeti letu la sauti ya Tan-ga na mtandao huu ambao tumeuan-zisha hivi sasa.

Umuhimu wa matangazo ya biashara

SAUTI YA TANGAMATANGAZO 11

TANGA URBAN WATER SUPPLY AND SEWARAGE AUTHORITY

P.o. Box 5011, Tanga TanzaniaPhone:255(0)272644626/7Email: uwsa-tanga@karibu tanga.com

[email protected] free numbers0752-0782800001 or 0713800252

SAUTI YA TANGA

MICHEZOSAUTI YA TANGA

Gazeti la SAUTI YA TANGA hutolewa na Tanga Publishers na kupigwa chapa na Business Printers Limited

Coming together is a BeginningKeeping together is ProgressWorking together is Sucess CONTACTS: HEAD OFFICE: Whole sale & Retail Jamhuri St.Sub-Whole Sale: 14 Sikukuu Msimbazi St.BRANCH: Haidery Plaza / Ground Floor.ADDRESS: P.o. Box 20073, DSM - TEL: 2117090 / 2117358 FAX: 2117357 MOBILE: 0713 325488E-MAIL: [email protected]

For all your school and office requirement