mifano ya kristo - everyday publications inc. titles cha zahabu 45 meza ya mkate wa onyesho 47...

60

Click here to load reader

Upload: trandieu

Post on 04-May-2018

531 views

Category:

Documents


36 download

TRANSCRIPT

Page 1: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MIFANO YA KRISTOkatika Agano la Kale

par W. A. Deans

EVERYDAY PUBLICATIONS INC.

310 Killaly Street West

Port Colborne, ON

Canada L3K 6A6Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.

Page 2: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

ISBN 978-88873-139-5

Publié originalement parEditions Evangéliques,

Nyankunde, Bunia, D.R. Congo

Imprimé au Canada

Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.

Page 3: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MAMBO YALIYO KITABUNI

UkurasaTangazo 5

Adamu, Mfano wa Kristo 7

Adamu (Sehemu ya pili) 9

Damu iliyovuja kwa Edeni 11

Kondoo ya Abeli 13

Safina ya Noa 15

Melkisedeki 18

Isaka (na Kondoo) 21

Yosefu 24

Kondoo ya Pasaka 26

Mana, Mkate toka Mbingu 29

Mwamba uliopasuka 32

Nyoka ya Shaba 35

Hema Takatifu 38

Mlango Mmoja 39

Mazabahu ya Shaba 40

Birika la Shaba 42

Kinara cha Zahabu 45

Meza ya Mkate wa Onyesho 47

Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49

Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51

Kuhani Mkubwa na Mavazi Matakatifu 54

Daudi na Kristo 57

Jumlisho 60

Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.

Page 4: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

4 MIFANO YA KRISTO

Mazabahu ya shaba, ona ukurasa 41.

Mazabahu ya kuchomauvumba, ona ukurasa 51.

Kinara cha zahabu, ona ukurasa 47.Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.

Page 5: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

TANGAZO

Biblia ni maandiko ambayo Mungu aliletea watu. Ina vitabu 66

ndani yake, vilivyo katika sehemu kubwa mbili. Sehemu hizi, ndizo

Agano la Kale na Agano Jipya, zinafungana kuwa moja. Sehemu moja

ya Biblia inatusaidia kufahamu sehemu ya pili.

Agano la Kale liliandikwa zamani sana, mbele ya kuzaliwa kwa

Bwana Yesu Kristo. Watu watakatifu waliongozwa na Roho Mtakatifu

kuandika maneno Mungu aliyotaka kujulisha watu.

Hata Agano la Kale liliandikwa mbele sana ya kuzaliwa kwa

Bwana Yesu, lina mifano mingi juu yake inayofanana naye katika

maisha yake, mauti yake, ufufuko wake, utumishi wake wa sasa na

utakatifu wake wa nyuma.

Kuna unabii kupasha habari za mambo yatakayotukia nyuma,

kutabiri vitu visivyotukia bado. Agano la Kale lina unabii juu ya Kristo

na vilevile mifano mingi ya ajabu juu yake. Mifano hii inaonekana

ndani ya maisha ya watu wa zamani, na katika mambo yaliyotukia juu

ya Waisraeli. Vilevile katika mambo ya hema ya kusanyiko jangwani

kuna maana nyingi za faida sana kueleza uzuri wa Kristo na utumishi

wake.

Mara nyingine matukio haya ya nyakati za zamani yanaonyesha

mifano ya Kristo waziwazi. Mara nyingine yanaonekana kama vivuli

kuonekana nusu nusu. Ni kama kivuli cha mtu kinachoonekana mbele

ya kufika kwake mwenyewe, kueleza namna yake kwa sehemu tu, si

wazi sana.

Kwa kuyafahamu kabisa tunahitaji kusoma Agano Jipya. Pale

mara nyingi maelezo ya mifano yanaonekana wazi kutufunulia maana

zao kabisa. Hivi tutatafuta mfano wa Kristo katika Agano la Kale, ha-

lafu tutapeleleza katika Agano Jipya kupata mashairi kueleza maana

yake.

5Copyright © 1973 Everyday Publications Inc.

Page 6: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Tutatumika na Biblia nzima pamoja na kitabu hiki kwa kufahamu

haki ya Mwokozi Yesu. Tuombe Mungu atuonyeshe Kristo katika mi-

fano hii. Tutashangaa na raha kwa kuona namna Agano la Kale linavy-

ofungana pamoja na Agano Jipya kutufunulia uzuri wa Kristo na

damani ya matendo yake.

Kama ukipenda Bwana Yesu na moyo wako, na ukiamini Neno

lake kabisa, utapata furaha kwa kusoma maelezo ya kitabu hiki.

Utajifunza maneno mengine mengi juu ya Mwokozi wako ambaye

unapenda.

Soma mashairi haya katika Biblia yako. Pale utafahamu Maandiko

Matakatifu yalitolewa na Mungu kwa njia ya mitume yake. Hata ma-

nabii ya zamani walitabiri juu ya Yesu. Soma mashairi haya :

2 Timoteo 3:16; 2 Petro 1:20-21; Yoane 8:56; Yoane 5:39,46; Zaburi

40:7; Waebrania 10:7; Matayo 22:45

6 MIFANO YA KRISTO

Page 7: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

ADAMU, MFANO WA KRISTO

(Mwanzo 1:26-28 ; 2:7,8,15)

Mbele ya kusoma juu ya Adamu kwa kitabu cha Mwanzo kwa Agano

la Kale, tutakumbuka kwamba hata kwa Agano Jipya tunasoma ya

kuwa Adamu alikuwa mfano wa Kristo atakayekuja (Waroma 5:14).

Kufanana kwake kuna tofauti vilevile.

Pale kwa kitabu cha Mwanzo (1:26-28; 2:7,8,15), tunaona Adamu

alikuwa umbo wa kwanza katikati ya watu. Mungu alimwumba na

mavumbi ya udongo, akafulisha pumuzi ya uzima puani mwake.

Adamu alikuwa nafsi ya uhai.

Kwa Agano Jipya tazama kwa 1 Wakorinto 15. Shairi 45 linasema

Adamu alikuwa umbo wa kwanza wa watu, mtu wa kwanza. Yeye

ndiye kichwa cha umbo wa kwanza.

Shairi 47 linaita Kristo “mtu wa pili.” Yeye ndiye kichwa cha

umbo mpya.

Mtu wa kwanza (Adamu) ni yule wa asili. Mtu wa pili ni yule wa

roho. Mtu wa kwanza (Adamu) alitoka katika dunia, mwenye udongo.

Mtu wa pili ni Bwana aliyetoka mbinguni (1 Wakorinto 15:47-48).

Hivi Adamu anafanana na Yesu kwa mfano, lakini kuna tofauti

vilevile.

Adamu alifanywa katika sura ya Mungu (Mwanzo 1:26). Kristo ni

sura ya Mungu asiyeonekana (2 Wakorinto 4:4; Wakolosayi 1:15)

kwani yeye ni Mungu mwenyewe katika mwili (1 Timoteo 3:16).

Adamu aliitwa Adamu wa kwanza. Kristo ni Adamu wa mwisho.

Kwa kuzaliwa kwa mwili sisi tulichukua sura (na tabia) ya Adamu wa

kwanza. Lakini kama tukizaliwa mara ya pili kwa Roho, kwa imani

katika Kristo, tutachukua sura ya Adamu wa mwisho. Tulivaa sura ya

mtu wa udongo, lakini katika Kristo tutavaa sura ya Mtu wa mbingu

7

Page 8: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

(1 Wakorinto 15:45-49). Soma vilevile 1 Yoane 3:2; Wafilipi 3:20-21.

Bwana Yesu alisema na Nikodemo, “Ila mtu azaliwe mara ya pili

hawezi kuona ufalme wa Mungu.” Na tena, “Kilichozaliwa kwa mwili

ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usishangae kwa sababu

nilikuambia, Sharti muzaliwe mara ya pill” (Yoane 3:3,6,7).

Katika Adamu tunariti hukumu ya mauti. Sisi tunaoamini Kristo

tunapata uriti wa uzima wa milele.

Angalia sasa katika Waroma. Tusome kwa Sura 5. Anza na shairi

15 mpaka 19. Katika mashairi haya tunaona maneno matano. Tunap-

ata katika:

1. Mtu mmoja (Adamu) KOSA na KUFA sh. 15

Mtu mmoja (Kristo) NEEMA na ZAWADI

2. Mtu mmoja (Adamu) HUKUMU na AZABU sh. 16

Mtu mmoja (Kristo) ZAWADI ya neema

(kuhesabiwa haki)

3. Mtu mmoja (Adamu) MAUTI sh. 17

Mtu mmoja (Kristo) UZIMA

4. Kwa kosa la mtu mmoja (Adamu) sh. 18

— watu wote walihukumiwa

Kwa tendo (msalaba) moja la haki (la Kristo)

— watu wote walipewa haki yenye uzima

5. Kwa kuasi kwa mtu mmoja (Adamu) sh. 19

— hali ya wenye zambi

Kwa kutii kwa mtu mmoja (Kristo)

— haki ya Mungu inapatikana

8 MIFANO YA KRISTO

Page 9: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

ADAMU

(Sehemu ya pili)

KUPATA MKE

Tunaendelea sasa kuonyesha namna Adamu alifanana na Kristo.

Mungu alimpa mke wake. Vivyo hivyo, Mungu alimpa Kristo Kanisa

kuwa mke wake.

Adamu alikuwa pekee katika shamba la Edeni. Nyama walikuwa,

na ndege, lakini msaidizi kwaye hakuwa. Mungu alisema, “Si vema

mtu awe peke yake; nitamfanyia msaidia anayefaa kwake” (Mwanzo

2:18).

Mungu akalalisha Adamu na usingizi, akaondosha mfupa mmoja

toka mbavu, akafunga mwili wake tena. Kwa ule mfupa Mungu aka-

jengea Adamu mke wake. Akampa kwa Adamu. Tazama Mwanzo 2:20-

22.

Adamu akasema, “Huyu sasa mfupa wa mifupa yangu, na nyama

ya nyama yangu; akaitwa Mwanamke kwa maana aliondoshwa katika

mume” (Mwanzo 2:23).

Vile kwa Kanisa, mke wa Kristo. Kwa njia ya usingizi mzito

(ndiyo mauti) Kristo alipata mke. Yeye alitobolewa, akakufia wenye

zambi. Juu ya kuumia kwake na mauti yake, Mungu amempa Kanisa.

Kanisa ni mwili wa Kristo — mifupa yake, mikono yake. Kristo

ni kichwa chetu, sisi tuko viungo vya mwili wake (Waefeso 1:22-23;

1 Wakorinto 12:27).

Kwa sura ya mbegu tunasoma kwa Yoane 12:24 juu ya kufa kwa

Kristo. Namna mbegu, ikibaki na uzima, inabaki pekee. Lakini ikain-

gia udongoni, ikakufa, inatoa mavuno ya mbegu nyingi. Kanisa lina-

toka ndani ya mauti ya Kristo na ufufuko wake.

9

Page 10: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kristo alipenda Kanisa na alijitoa kwa ajili yake (Waefeso 5:23-27).

Hivi Kanisa ni bibi ya Kristo, ndio watu walioletwa kwake na Baba

yake (Yoane 17:24).

KUTAWALA

Mungu aliwapa Adamu na mke wake ruhusa kutawala juu ya

kila kiumbe kilichokuwa hai. Adamu alifuga nyama zote (Mwanzo

1:26-28).

Kristo anatolewa enzi. Atasimama Mfalme wa wafalme. Adui zake

watakuwa kiti cha miguu yake (Ufunuo 11:15; Zaburi 72:8; Zekaria

9:10) .

Enzi yake itaenea duniani pote. Atatawala na fimbo ya chuma.

Mke wake, ndilo Kanisa, atatawala pamoja naye (Ufunuo 2:26-27;

3:21; 20:6). Kila kiumbe kitawekwa chini ya enzi ya Kristo (Zaburi

8:3-9). Kila ulimi utakiri ya kuwa Yesu ni Bwana kwa utukufu wa

Mungu Baba (Wafilipi 2:9-11).

Utawala wa Adamu shambani la Edeni unafanana na utawala wa

Kristo duniani pote.

10 MIFANO YA KRISTO

Page 11: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

DAMU ILIYOVUJA KWA EDENI

Mungu alimpa Adamu ruhusa kula matunda yote ya shamba la Edeni

ila tunda la mti mmoja. Mti ule uliitwa “mti wa kujua uzuri na ubaya.”

Mungu alisema kama wakiasi wakikula tunda la mti ule, watakufa

(Mwanzo 2:9, 17).

Shetani alifika mbele ya Hawa, mke wa Adamu, kumjaribu. Ali-

fika na mwili wa nyoka, kusemezana na lugha ya watu. Alizarau

masemo ya Mungu na agizo lake. Alijaribu Hawa ale tunda hili.

Hawa alifahamu agizo la Mungu. Alisema na nyoka, “Mungu

amesema: Musile (matunda) yake wala musiyaguse, musife” (Mwanzo

3:3).

Lakini Shetani alidanganya Hawa. Mke yule akatazama matunda

ya ule mti, akayatamani, akachukua ya matunda yake, akampa mume

wake vilevile pamoja naye (Mwanzo 3:6). Wao wote wawili waka-

anguka kufanya zambi. Hawa alidanganywa, Adamu alikula na kusudi

(1 Timoteo 2:14).

Ahadi ya Mungu juu yao ilikuwa hivi: Mukikula, mutakufa. Sasa

Adamu na Hawa wanatambua ya kuwa walikuwa watupu. Wakatafuta

njia ya kujifunika kwani waliogopa Mungu. Wakashona majani kuvaa.

Wakajificha, Mungu asiwakute. Walikuwa wenye zambi.

Kisha Mungu aliwatafutatafuta. Akawakuta, wakifichama katikati

ya miti ya shamba. Kwa kukiri zambi yao mbele ya Mungu, Adamu

alichongea mke wake. Hawa alichongea nyoka. Sasa hukumu inawa-

ngojea.

Lakini kwa neema yake Mungu aliwapatia njia ya ukombozi.

Mauti waliyostahili kupata iliangukia nyama waliochinjwa na Mungu.

Damu ilivuja katika Edeni! Hivi Mungu aliwavalisha na mavazi ya

ngozi. Yeye mwenye huruma aliwapa njia ya ukombozi.

Pale tunapata mfano mwingine wa Kristo. Ngozi hizi zilipatikana

11

Page 12: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

kwa njia ya mauti ya nyama. Damu ya ukombozi ilimwangika. Majani

waliyoshona kuwa mavazi hayakutosha. Kisha, Mungu aliwavalisha

na ngozi. Wakati Mungu alipotazama Adamu au Hawa, aliona alama ya

ukombozi, ukumbusho wa damu. Hivi, hata walihukumiwa kwa njia ya

kulima na jasho na mke kuzaa na taabu, hata walifukuzwa toka Edeni,

mauti iliwekwa kando kwa ajili ya damu. Walipata wakati wa kuishi

mbele ya kufariki, lakini Mungu aliwazuiza wasiingie tena shambani

kula tunda la uzima. Hawakustahili tena (Mwanzo 3:24).

Wenye zambi leo wanajaribu kubembeleza Mungu na majani ya

matendo yao, wakiwaza wataponea hukumu ya mauti. Lakini “Msha-

hara wa zambi ni mauti” (Waroma 6:23). Soma vilevile Ezekieli 18:20,

“Nafsi inayofanya zambi itakufa.”

Mungu ametengeneza njia ya wokovu! Mwana wake, Yesu Kristo,

kama nyama katika Edeni, alikufa kwa ukombozi kwa wenye zambi.

Damu yake ilivuja kulipa deni ya zambi. Mtu anayetaka kuokolewa,

apokee Yesu kuwa Mkombozi wake. Hivi atapatana na Mungu kwa

salama.

12 MIFANO YA KRISTO

Page 13: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

KONDOO YA ABELI

(Mwanzo 4:1-15)

Mzaliwa wa kwanza duniani alikuwa mwuaji. Kaina, mwana wa

kwanza wa Adamu na Hawa, aliua Abeli, mdogo wake.

Wakati Adamu na Hawa walipokosa katika Edeni, walijaribu ku-

ficha utupu wao na majani ambayo walishona. Lakini Mungu haku-

kubali matendo yao kufunika zambi. Alitaka damu kumwangika. Hivi

walifunikwa na ngozi za nyama za ukombozi.

Watoto wao, ndio Kaina na Abeli, walijua lazima damu ivuje kwa

kupata salama na Mungu. Tusiwaze ya kwamba Kaina alikuwa mwenye

zambi kuliko Abeli. Wao wote wawili walikuwa wenye zambi, walihitaji

usamehe.

Tofauti katikati yao ilikuwa namna ya matoleo yao. Kwa

kuwakubali au kuwakataa, Mungu alitazama matoleo yao.

Kaina alichagua matunda ya udongo kuwa sadaka mbele ya

Mungu. Lakini udongo ulilaaniwa (Mwanzo 3:17); toleo haliwezi ku-

toka pale. Lilifanana na majani Adamu aliyoshona kujaribu kufunika

utupu wake kwa Edeni. Hayakufaa. Ilikuwa sadaka pasipo damu.

Hata Kaina aliwaza ya kuwa mboga, matunda, maua ya umalidadi

yataweza kupendeza Mungu, hakukuwa vile. Hata alifikili Mungu ata-

furahia matunda ya kazi yake ya mlimaji, alianguka kwa mawazo. Njia

moja kufikia Mungu ilikuwa njia ya ukombozi, njia ya damu.

Abeli alikuwa mlinzi kondoo. Akachukua mwana-kondoo katika

kundi kuchinja sadaka mbele ya Mungu. Akamtoa pamoja na mafuta,

zabihu kwa Mungu.

Mungu hakutazama Kaina wala Abeli. Macho yake yalipita juu

ya sadaka. Mungu alikubali zabihu ya Abeli, yenye damu. Mungu

alikataa toleo la Kaina lisilo na damu (Mwanzo 4:4-5).

13

Page 14: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kaina alikataliwa kwa ajili ya sadaka isiyofaa. Alikosa imani; ali-

jaribu kufikia Mungu kwa njia ambayo alitunga mwenyewe.

Abeli alikubaliwa kwa ajili ya sadaka ya kumpendeza Mungu.

Alitoa zabihu ya damu, kwa imani (Waebrania 11:4).

Mungu akahamakia Kaina, akamwonyesha njia ya kupokelewa. Ni

kutoa sadaka ya kufaa apate usamehe; kama sivyo, zambi itabaki

(Mwanzo 4:7).

Lakini Kaina hakutaka. Akaamukia ndugu yake, akamwua. Mungu

akamwekea chapa. Kaina akatoka kutangatanga duniani, kujulikana

kuwa mwenye zambi pahali po pote.

Kondoo ya Abeli ni mfano wa Kristo. Kristo ni kondoo safi ya

Mungu. Wakati Yoane Mbatizaji alipoona Yesu akikuja kwake,

akasema, “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu anayechukua zambi ya

ulimwengu” (Yoane 1:29-30).

Kama mwana-kondoo anayepelekwa kuchinjwa, na kama kondoo

anavyonyamaza mbele yao wanaokata manyoya yake, Yesu hakufu-

ngua kinywa chake (Isaya 53:7).

Mwenye zambi leo anayetaka kupatana na Mungu, sharti awe na

imani juu ya sadaka ya Kristo msalabani. Damu ya Yesu, kama ya

mwana-kondoo, ni njia ya ukombozi, ndiyo njia ya usamehe kwa

zambi.

“Mumekombolewa, si kwa vitu vinavyoharibika ... lakini kwa

damu ya damani, kama ya kondoo asiye na kilema wala alama, damu

ya Kristo” (1 Petro 1:18-19).

Kama Mungu hakutazama Kaina au Abeli, lakini zaidi matoleo

yao, vivyo hivyo Mungu hatazami sisi, lakini sadaka ambayo tuna-

mtolea kwa kumkaribia.

Kaina akifika na matunda ya udongo, alikataliwa. Abeli akifika na

kondoo, akimwanga damu yake, alikubaliwa.

Sisi kujaribu kupendeza Mungu na matendo yetu ni bule. Lakini

kwa kuamini Yesu Kristo, Kondoo ya Mungu, aliyejitoa msalabani kwa

ajili yetu, tunapata usamehe wa zambi. Tutakubaliwa na Mungu kwa

milele.

14 MIFANO YA KRISTO

Page 15: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

SAFINA YA NOA

(Mwanzo 6-9)

Ilikuwa watu hawajaona bado mvua duniani. Tangu mwanzo maji ya-

litoka katika chemchemi za udongo. Hivi watu walizihaki Noa wakati

alipowapasha juu ya hatari ya tufani. Walimchekelea wakati alipojenga

safina mbokani, mbali na mito ya maji.

Uovu ulizidi duniani. Mawazo ya watu yalikuwa mabaya tu siku

zote. Dunia iliharibika mbele ya Mungu (Mwanzo 6:5,11-13). Mungu

alisema, “Roho yangu haitashindana na mtu milele” (sh. 3). Alikusudi

kuharibu watu kwa garika ya maji. Alipasha ya kuwa watu na nyama

na ndege watazama, watakufa (Mwanzo 6:17).

Uovu wa dunia ya leo ni sawa. Watu hawataki kuogopa hukumu ya

Moto ambayo Mungu anayokusudi kuleta juu ya zambi.

Mungu aliwaza kuonyesha rehema kwa Noa, mtu wa haki. Noa

alitembea pamoja na Mungu, kama Enoka (Mwanzo 5:24; 6:8-9). Hivi

Mungu alitunga njia ya wokovu. Aliagiza Noa ajenge safina. Ali-

mwonyesha kipimo chake kwa urefu na upana na urefu juu. Alimwo-

ngoza kuweka dirisha moja juu, na mlango mmoja, kwa kuingia.

Alimwagiza kupakaa safina ndani na inje kwa lami (kama kasuku).

Noa alitii (Mwanzo 6:19-20).

Kwa wakati wa sasa, kama zamani, Mungu anatangaza njia ya

wokovu kwa neema, kwa watu walio katika hatari ya hukumu. Ana-

pasha habari ya Safina ya sasa, ndiye Kristo, pahali mwamini atakapo-

jificha na amani katika zoruba ya moto kwa kuja.

Noa alitangaza hatari ya hukumu kwa watu kwa wakati wake.

Alikuwa mhubiri wa haki (2 Petro 2:4-5). Alihubiri hukumu na

wokovu.

15

Page 16: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Noa na wana wake (Semu, Hamu na Yafeti) walidumu kujenga sa-

fina kubwa namna Mungu alivyowaagiza. Hata watu walizarau, Noa

alihubiri na alidumu kwa kujenga. Kazi ilitimia, ilikwisha.

Noa na jamaa yake, wote watu wanane, waliingia ndani ya safina,

kwa imani (Waebrania 11:7). Nyama namna zote na ndege wakaingia.

Mungu mwenyewe akawafunga ndani. Mlango ulifungwa (Mwanzo

7:16).

Kwa wakati wa sasa wahubiri wanatangaza hatari ya hukumu juu

ya zambi. Wanapasha habari ya kutokea kwa Mwana wa Mungu.

Lakini kama kwa wakati wa Noa, leo watu wanaendelea katika zambi.

Hawataki kupokea neema ya Mungu na kuingia ndani ya Kristo, Safina

yetu (2 Petro 2:5).

Basi, wakati Noa alipoingia ndani ya safina, mvua ikaanza kunye-

sha. Maji yalitokatoka katika udongo, chemchemi zilijaa. Udongo

ulianza kujaa na tufani kuwa garika kubwa ya kumeza dunia pia.

Watu waliokuwa wakizihaki, wale wasioamini, walibaki inje.

Walianza kukimbiakimbia juu ya vilima. Labda wengine waligonga

mlango wa safina, wakitaka kuingia. Lakini wakati wa wokovu uli-

kuwa umepita. Watu walikufa wote, na nyama zote, na ndege (Mwanzo

7:21-23). Wale waliokuwa ndani ya safina —watu na nyama na ndege

— walipona wote.

Tunaona safina ya Noa ni mfano wa Kristo. Watu walioingia ndani

ya safina waliishi kwa amani. Njia ya wokovu ilikuwa safina tu.

Haikuwa nyingine. Mlango ulikuwa mmoja tu kupata raha (Mwanzo

6:16; Yoane 10:9).

Safina ilipokea uzito wa tufani juu yake. Zoruba ilipiga na nguvu

lakini safina ilipata ukali wake; watu walioingia walipona pia. Kwa

hivyo Bwana Yesu amebeba hasira ya Mungu sisi tuliyostahilia kupata.

Gazabu ya hukumu ilimwangukia. Alitukomboa. Yeye ni Mkombozi

wetu. Kwa imani tunaishi kwa amani ndani yake, kwa milele.

Nyuma ya garika wakati maji ya tufani yalipoanza kupunguka, sa-

fina ilikwama juu ya Mlima Ararati. Wakatoka wote. Noa akajenga

mazabahu (Mwanzo 8:1-5). Akatoa sadaka za sifa mbele ya Mungu

(Mwanzo 8:20-22). Mungu akaweka upindi wa mvua winguni, alama

ya agano katikati ya Mungu na watu. Hataharibu tena dunia kwa maji

16 MIFANO YA KRISTO

Page 17: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

(Mwanzo 9:8-17). Hukumu ya nyuma itakuwa kuharibu dunia kwa

moto (2 Petro 3:4-14).

“Kama lalo inavyoshuka upande mmoja wa mbingu na kungaa

hata upande mwingine wa mbingu, ndivyo Mwana wa watu

atakavyokuwa katika siku yake . . . Kama ilivyokuwa siku za Noa, ndi-

vyo itakavyokuwa siku za Mwana wa watu. Walikula, walikunywa,

walioa, waliolewa hata siku ile Noa alipoingia katika safina, na garika

ilifika ikawaangamiza wote” (Luka 17:24, 26, 27).

Safina ya Noa 17

Page 18: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MELKISEDEKI

(Mwanzo 14 :17-24)

Melkisedeki ni mfano wa Yesu Kristo, Mfalme na Kuhani Mkubwa.

Mtu yule aliishi zamani kwa wakati wa Abrahamu (Abramu). Alikuwa

mfalme wa Salemi (nyuma yake mji ule uliitwa Yerusalema). Alikuwa

vilevile kuhani la Mungu aliye juu (Mwanzo 14:18).

Melkisedeki alikuwa mtu, lakini Biblia haituonyeshi habari za

wazazi wake. Mambo ya kuzaliwa kwake na uzazi wake yalifichwa

kusudi awe mfano wa Kristo aliyezaliwa kwa ajabu, bila baba duniani

na mama bikira.

Soma maneno ya Melkisedeki katika Mwanzo 14:17-24. Wafalme

wane walipiga vita na wafalme watano (sh. 9), halafu wafalme wa

Sodomo na Gomora walikamatwa. Wafalme washindaji walichukua

mali zote za Sodomo na Gomora, na vyakula vyo vyote na watu. Wa-

likwenda vilevile na Loti, mwana wa ndugu ya Abrahamu, aliyekaa

katika Sodomo (mash. 10-12).

Abrahamu akasikia habari hizi, akakusanya watu wa nyumba yake,

na watumishi wake (wote watu 318), akafuata wale adui. Akawakuta,

akapigana nao, akawashinda. Kwa hivi Abrahamu alinyanganya mali

zote za nyara, na kurudisha Loti na mali zake na watu (mash. 13-16).

Kwa kurudi toka vita na nyara zake, Abrahamu alikutana na

Melkisedeki aliyetokea mbele yake. Yule mfalme wa Salemi, kuhani la

Mungu aliye juu, akatoa mkate na mvinyo. Melkisedeki akabariki

Abrahamu katika jina la Mungu aliye juu. Abrahamu akimpa zaka ya

moja ya kumi katika vyote alivyopata (sh. 20).

Vilevile mfalme wa Sodomo alitokea mbele ya Abrahamu. Ali-

mwambia arudishe tu watu, abaki na mali zote. Lakini Abrahamu

18

Page 19: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

alikataa kupokea kitu kimoja mikononi mwa mfalme wa Sodomo, asi-

jisifu kusema alitajirisha Abrahamu (sh. 23).

Hivi Abrahamu alichagua katikati ya wafalme wale wawili:

Melkisedeki (mfalme wa Salemi, kuhani la Mungu aliye juu) na

mfalme wa Sodomo. Alichagua Melkisedeki. Alipokea zawadi yake na

baraka yake. Alitoa zaka yake kwake. Lakini alikataa zawadi za mfa-

lme wa Sodomo, mji mwovu.

Tunapata maelezo ya mfano wa Melkisedeki kwa Waebrania 6:20;

7:1-28. Angalia namna Kristo anavyofanana na Melkisedeki.

A. Kuzaliwa kwa Yesu ni ajabu. Maneno ya kuzaliwa kwa Melki-

sedeki yanafichwa. Baba na mama yake hawajulikani, wala mwanzo

wake au mwisho wake. Hivi alifanana na Yesu, Mwana wa Mungu,

aliyezaliwa kwa ajabu bila baba duniani, na mama yake bikira (Wa-

ebrania 7:3).

B. Kristo ni Mfalme. Melkisedeki alikuwa mfalme wa haki,

mfalme wa Salemi (maana mfalme wa Salama) (Waebrania 7:2). Kristo

ni Mfalme:

— Herode nyuma ya kuzaliwa kwa Yesu alimtaja “Mfalme wa

Wayuda” (Matayo 2:2).

— Manabii walitabiri (Matayo 21:4-5; Zaburi 2:8; Danieli 7:13-14)

— Pilato alimwuliza, “Wewe mfalme basi?” (Yoane 18:37; 19:14-

15)

— Mfalme wa wafalme (Ufunuo 17:14; 19:16; 1 Timoteo 6:15)

C. Kristo ni Kuhani Mkubwa kuliko (Waebrania 7:1-28). Kristo

alizaliwa katika kabila la Yuda, si katika kabila la Lawi lililotolewa

ukuhani (Waebrania 7:5,14). Haruni, kuhani mkubwa wa kwanza,

alikuwa Mlawi, na wote ambao walimfuata katika ukuhani walikuwa

Walawi.

Lakini Melkisedeki, kuhani la Mungu aliye juu, aliishi mbele ya

kuzaliwa kwa Lawi. Wakati Abrahamu alipojinyenyekeza mbele ya

Melkisedeki akitoa zaka kwake, ni kama Lawi atakayezaliwa kwa

uzazi wa Abrahamu. Alianguka mbele yake (ndani ya Abrahamu). Hivi

ni wazi, mkubwa alikuwa Melkisedeki, si Lawi. Soma Waebrania 7:2.

Melkisedeki 19

Page 20: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Mungu ametia Yesu Kristo kuhani kwa milele kwa daraja la

Melkisedeki (Waebrania 6:20; 7:17, 21). Makuhani wengine wanaku-

fakufa, lakini yeye anaishi milele kuombea watu wake (mash. 15-16).

D. Agano la Kuhani Mkubwa Kristo linapita agano la makuhani yaWalawi (Waebrania 7:22) :

— Kristo ni Mpatanishi wa agano linalosimamishwa juu ya ahadi

zinazozidi kwa uzuri (Waebrania 8:6)

— Ni Agano Jipya (Waebrania 8:7-8)

Makuhani wote wa daraja la Lawi walihitaji kutoa kwanza sada-

ka kwa zambi zao wenyewe. Lakini Kuhani Yesu Kristo hana

zambi. Alijitoa mara moja kwa ajili ya wenye zambi kutupatia

wokovu kwa milele (Waebrania 7:23-28).

— Hakuna ukumbusho tena wa zambi kamwe (Waebrania 8:12-

13; 10:17-18)

Soma vile Waebrania 10:9-18 kwa kupata shangwe juu ya kazi

kamilifu ya Mwokozi Yesu, ndiye Sadaka yetu, Kuhani Mkubwa wetu,

Mfalme wetu.

20 MIFANO YA KRISTO

Page 21: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

ISAKA (NA KONDOO)

(Mwanzo 22:1-44)

Katika habari za Abrahamu na Isaka tunapata mfano wa Mungu

mwenyewe akikubali kutoa mwana wake wa pekee. Lakini vilevile tu-

napata mfano wa Kristo kwa kondoo ndume ambaye Mungu alimleta

kuwa mkombozi kukufilia Isaka.

Hivi tuseme tuna mifano miwili ya Kristo katika matukio ya ma-

neno ya sadaka ya Abrahamu wakati alipotii Mungu kwa kutoa mwana

wake kuwa zabihu ya kuteketezwa.

Tuanze kwanza juu ya Isaka, mwana mpendwa wa baba Abra-

hamu.

Katika Mwanzo 22, shairi 2, kitabu kinaita Isaka “mwana wako,

mwana wako wa pekee ambaye unampenda, hata Isaka.” Isimaeli,

mwana wa Hagari, Mungu hakuhesabu kwani ahadi yake kwa Abra-

hamu ilikuwa juu ya mwana wake wa utaratibu, ndiye Isaka. Alimwa-

giza kutoa mwana huyu wa ahadi kuwa sadaka ya kuteketezwa.

Abrahamu anafanana na Mungu Baba. Isaka anafanana na Yesu,

Mwana Mpendwa wake. (Tazama Marko 1:11). Abrahamu hakukataa

kuchinja mwana wake kuwa zabihu. Mungu Baba hakuachilia Mwana

wake, lakini alimtoa kabisa badala yetu sisi sote (Waroma 8:32).

Isaka, mtoto wa ahadi, anafanana na Kristo, mtoto wa ahadi. Soma

Mwanzo 17:16; Mwanzo 3:15; Isaya 7:14.

Kuzaliwa kwa Isaka kulikuwa ajabu, vile kuzaliwa kwa Kristo.

Abrahamu na Sarai walikuwa wazee. Wakati wa kuzaa ulipita

mbali (Mwanzo 18:13). Lakini yule mama mzee alichukua mimba,

akazaa mtoto wake wa kwanza.

Mastaajabu juu ya kuzaliwa kwa Kristo. Baba yake ni Mungu

mwenyewe. Roho ya Mungu alikuja juu ya Maria akiwa bikira, akazaa

Kristo bila kujua mwanamume.

21

Page 22: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kuzaliwa kwa Isaka kulifuata utaratibu wa unabii. Vile Kristo

(Mwanzo 21:2; Wagalatia 4:4).

Jina la Isaka lilitajwa mbele ya kuzaliwa kwake (Mwanzo 17:19).

Vilevile, jina la Kristo (Matayo 1:21).

Isaka, mwana mpendwa wa baba yake, alimtii. Wakati Abrahamu

aliposhika njia kwenda kutoa Isaka juu ya kilima Moria, mwana ali-

kwenda pamoja naye akiwa na roho ya kutii (Mwanzo 22:3-6).

Ushirika katikati ya baba Abrahamu na mwana Isaka ulionekana wazi.

Bwana Yesu alisema, “Baba hakuniacha peke yangu, sababu ni-

nafanya saa zote maneno ambayo yanampendeza” (Yoane 8:29).

Abrahamu aliamini Mungu. Hata kama Isaka atakufa, sharti

Mungu atimize ahadi yake. Hivi Abrahamu aliwaambia watumishi,

“Mukae hapa pamoja na punda, nami na kijana tutakwenda kule; na

tutaabudu na kurudi tena kwenu” (sh.5).

Katika ushirika Abrahamu na Isaka walipanda kilima kutayarisha

toleo. Abrahamu akajenga mazabahu pale, akatandika kuni, akafunga

Isaka, mwana wake, akamweka juu ya mazabahu juu ya kuni. Abra-

hamu akanyosha mkono wake, akatwaa kisu achinje nacho mwana

wake.

Kweli, hapa tunapata sura ya msalaba. Baba Mungu alitoa Mwana

wake mpendwa wa pekee. Damu yake ilivuja. Yesu alikufa kuwa toleo

kwa zambi.

Sauti ya malaika ilizuiza Abrahamu asiue Isaka. Lakini kule kwa

Kalvari Mungu alinyamaza kimya. Hakuponyesha Mwana wake

mpendwa. Hakuachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote

(Waroma 8:32).

Kwa habari za Abrahamu, Isaka alinyakuliwa toka mauti kuwa sura

ya Yesu katika ufufuko wake. Kufika pale kweli Isaka ni mfano wa

Kristo.

Lakini sasa tunaangalia mfano wa pili katika habari hizi. Wakati

Isaka alipouliza baba yake mbele, “Tazama moto na kuni; lakini wapi

mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?” (sh.7), Abrahamu aka-

jibu, “Mungu atajipatia mwenyewe mwana-kondoo kwa sadaka ya

kuteketezwa” (sh.8).

22 MIFANO YA KRISTO

Page 23: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Hivi sasa, kweli kondoo ndume ameonekana, akafungwa na pembe

zake katika kichaka (sh.13). Mungu alimpatia kondoo kuwa mko-

mbozi. Isaka alifunguliwa. Amepona!

Abrahamu akakwenda, akatwaa yule kondoo ndume, akamtoa kwa

sadaka ya kuteketezwa badala ya mwana wake (sh.13).

Kondoo huyu ni mfano wa Kristo vilevile. Damu ya Yesu ilivuja

kwa ukombozi wa wenye zambi.

“Mumekombolewa, si kwa vitu vinavyoharibika . . . lakini kwa

damu ya damani, kama ya kondoo asiye na kilema wala alama, damu

ya Kristo” (1 Petro 1:18-19).

Isaka 23

Page 24: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

YOSEFU

(Mwanzo 36-50)

Habari za maisha ya Yosefu zinakula sura nyingi katika Biblia. Lakini

msomaji atakayedumu kupeleleza habari hizi atapata faida nyingi.

Mtafutaji atakuta mambo mengi ya damani na mifano juu ya Kristo.

Nafasi inatukosa kwa kutaja mifano yote. Tutaonyesha maneno

machache tu.

Yosefu alipendwa sana na baba yake (Mwanzo 37:3). Yesu ni

Mpendwa wa Mungu (Matayo 3:17; 17:5; Yoane 10:17).

Yosefu, mchungaji wa kondoo (37:2), anafanana na Yesu, Mchu-

ngaji Mwema aliyetoa uzima wake badala ya kondoo zake (Yoane

10:11).

Yosefu alichukia zambi za ndugu zake. Alifahamisha baba yao

mambo ya uzalimu wao (37:2). Bwana Yesu alichukia zambi lakini

alifika hapa duniani kuokoa wenye zambi (1 Timoteo 1:15).

Ndugu zake Yosefu walimchukia (Mwanzo 37:4, 5, 8). Ndugu zake

Yesu walimzarau (Luka 4:28-29; Yoane 8:40; 15:25; Yoane 7:5). Kwa

Yosefu na kwa Yesu ndugu zao walikuwa na uwivu juu yao (Mwanzo

37:11; Matayo 27:17-18; Marko 12:6-7).

Kama Bwana Yesu alivyotumwa na Baba toka mbinguni kwa watu

wake, vivyo hivyo Yosefu alitumwa na baba yake karibu na ndugu zake.

Lakini walimbeua, wakamkataa (Mwanzo 37:13-14,18; Yoane 1:11) .

Ndugu za Yosefu na taifa la Yesu walishauri kuwaua (Mwanzo

37:18; Matayo 12:14). Walizihaki Yosefu, wakimwondoshea mavazi

yake (Mwanzo 37:23). Kwa Yesu vivyo hivyo (Matayo 27:27-28;

Yoane 19:23).

Ndugu zake Yosefu wakamwuza kwa Waisimaeli kwa vipande 20

vya feza (Mwanzo 37:28) . Hesabu juu ya Yesu ilikuwa bei ya mtumwa

katika Israeli (Zekaria 11:12), ndiyo vipande 30 vya feza (Matayo

26:14-15; 27:3, 9).

24

Page 25: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Vazi la Yosefu lilichovya katika damu kuonyesha mfano wa mauti

(Mwanzo 37:31), wadanganye baba zao awaze nyama mkali wa poli

amemwua. Lakini Waisraeli waliua Yesu kabisa, damu yake kuvuja

kwa kukomboa wenye zambi na hukumu ya Mungu (Matendo 2:22-

23; Waebrania 9:14-15; Waroma 5:8-9).

Yosefu aliwekwa ndani ya shimo la birika bila maji. Nyuma

wakampandisha tena hai (Mwanzo 37:24,28). Pale tunafikili mfano wa

kuzikwa na ufufuko wa Yesu (1 Wakorinto 15:3-4).

Yosefu alikuwa mfano wa Yesu vilevile wakati alipotumikia Poti-

fari katika Misri. Alikuwa mtumwa wa heri, mwenye kutii, kujitenga

na zambi (Mwanzo 39:1-6; Wafilipi 2:5-8; Isaya 52:13). Wakati Yosefu

alipojaribiwa na mke wa Potifari, alikataa (Mwanzo 39:7-20). Bwana

Yesu alikuwa bila zambi kwa wazo wala tendo (1 Petro 2:22; 2 Wako-

rinto 5:21).

Unabii ulionyesha ya kuwa Yosefu atapata enzi kutawala juu ya

jamaa yake (Mwanzo 37:7, 9-10). Hivi, nyuma ya mateso (Mwanzo

39:20), Yosefu aliondoshwa pale katika gereza (mnyororo), ali-

heshimiwa, aliwekwa juu ya kiti cha enzi kutawala katika Misri

(Mwanzo 41:38-44).

Yesu atatimiza mfano huu kwani unabii juu yake umeandikwa,

“Utawala utakuwa juu ya bega lake” (Isaya 9:6-7). Jina lake linapita

kila jina (Wafilipi 2:9-11; 1 Wakorinto 15:25).

Yosefu alikuwa mwenye kusaidia ndugu zake wakati wa njaa. Kwa

neema, hata walimtesa, alisamehe zambi zao. Aliwakulisha katika

mahitaji yao. (Soma katika Mwanzo, Sura 41). Bwana Yesu alifikia

watu wake lakini walio wake hawakumpokea. “Lakini wote ambao

walimpokea aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, ndio wale

walioamini jina lake” (Yoane 1:12).

Habari Yosefu alizowapa watu wa kumtambua kwa neema zi-

likuwa: “Yosefu anaishi hata leo, naye ni mtawala” (Mwanzo 45:26).

Habari zetu tunaoamini Yesu kutangaza ni: Yuko hai, jina lake

linatukuzwa, ni mwenye neema. Kuja kwake kuokolewa, watu wa

kufa. Uzima mutapata kwake. Yeye ni MFALME WA WAFALME NA

BWANA YA WABWANA (Ufunuo 19:16).

Yosefu 25

Page 26: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

KONDOO YA PASAKA

(Kutoka 12)

Katika mifano ya Kristo kwa Agano la Kale hakuna mfano mwingine

unaopita kondoo ya pasaka kwa kuonyesha wazi maana ya Kalvari.

Kondoo ya pasaka alichinjwa kuwa mkombozi wakati Mungu

alipokusudi kuhukumu Misri na mauti. Lakini alisema, “wakati ni-

takapoona damu, nitapita juu yenu” (Kutoka 12:13). Elfu za watu

walipona na elfu za wengine waliuawa.

Neno hili lilitokea nyuma ya kufa kwa Yosefu. Kwa wakati wa

maisha yake Waisraeli waliishi vizuri. Farao alipenda Yosefu na jamaa

yake. Aliwapa sehemu ya inchi, ndiyo Goseni, kwa pahali pa kupanga.

Pale walilinda ngombe, walipata vyakula vya kutosha.

Lakini nyuma ya kufa kwa Yosefu Farao mwingine asiyejua Yosefu

alianza kutawala. Alipata hasira na hasidi juu ya Waisraeli, akawageuza

kuwa watumwa wa Wamisri. Walipiga matofali, walitumika kazi ya

nguvu bila mshahara, waliteswa zaidi. Farao aliwaogopa vile, hivi ali-

agiza waue watoto wanaume wote wakati wa kuzaliwa kwao. Wa-

sichana tu waache hai.

Kwa huruma Mungu aliamusha mwongozi kwa Israeli. Alikuwa

Musa aliyesikia sauti ya Mungu jangwani wakati aliposemezana naye

toka kijiti uliowaka moto bila kuteketea.

Hivi Musa alitokea mbele ya Farao kuomba uhuru kwa Waisraeli.

Farao alikataa. Kwa kulipa kisasi, Mungu alituma mapigo juu ya inchi

ya Misri na juu ya Farao mwenyewe. Lakini roho yake ilikuwa ngumu

kama jiwe.

Katika mapigo tisa Mungu aligeuza maji kuwa damu, alituma

vyula, chawa, mainzi, ugonjwa katikati ya nyama, majipu, mvua ya

mawe, nzige na giza. Farao alibaki na roho ngumu; hakukubali kuwapa

26

Page 27: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Waisraeli uhuru. Hivi Mungu alikusudi kupiga Misri na pigo la kumi,

ndilo mauti.

Mungu alitangaza kusudi lake la azabu (Kutoka 12:12,23).

Alisema, “Nitapita katika inchi ya Misri usiku ule, na nitapiga waza-

liwa wa kwanza wote, mtu na nyama vilevile.” Alipasha mbele juu ya

hukumu ya mauti.

Vilevile Mungu, kwa neema, alitangaza njia ya kuponea hukumu.

Ilikuwa hivi sababu ya kufa kwa mkombozi. Aliagiza kila mtu atwae

mwana-kondoo kwa jamaa yake. Ilimpasa kuwa ndume ya mwaka wa

kwanza, pasipo kilema. Sharti ndume awekwe muda wa majuma mawili

kuonyesha usafi wake, halafu wamchinje mangaribi (Kutoka 12:3-6).

Pale tunapata mfano safi wa Kristo. Leo wenye zambi duniani pote

wanastahili hukumu ya Mungu, ndiyo mauti. Lakini Mungu amete-

ngeneza njia ya wokovu. Ilipasa Kristo anayeitwa “Mwana-kondoo wa

Mungu” (Yoane 1:29) kufa kuwa Mkombozi wa watu. Kondoo aliye-

kufa katika Misri anafanana na Bwana Yesu aliyekufa msalabani kwa

ukombozi wetu.

Kondoo katika Misri alikuwa bila kipako, ndume safi. Vivyo

hivyo, Kristo alikuwa bila laumu au kipako (1 Petro 1:19; 2:22).

Hakustahili kufa, lakini alikufa “mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,

ili atulete kwa Mungu” (1 Petro 3:18).

Hata kwa kila nyumba au jamaa na jirani yake kondoo alichinjwa

kwa wakati wa Musa, Mungu hakufikili juu ya kondoo wengi, lakini

aliona kondoo zote kama mmoja tu (Kutoka 12: 3-5). Kwaye kondoo

zote walifanana na kondoo mmoja wa pekee, ndiye Yesu Kristo.

Mungu aliagiza Waisraeli kukamata damu ya kondoo aliyechin-

jwa, ndani ya bakuli, na kuitia juu ya nguzo mbili za kando ya mlango

na juu ya kizingiti cha juu (Kutoka 12:7). Alisema, “Damu itakuwa

alama kwenu juu ya nyumba pahali mutakapokuwa; na wakati ni-

takapoona damu, nitapita juu yenu, wala pigo halitakuwa juu yenu

kuwaharibu ninyi; wakati nitakapopiga inchi ya Misri” (sh. 13).

Hivi Waisraeli walichinja kondoo, walipakaa damu yake mla-

ngoni, kwa imani. Walibaki nyumbani kula nyama ya kuchomwa ya

kondoo namna Mungu alivyowaagiza. Walikula kwa haraka, wakiwa

na fimbo mikononi, viatu miguluni, tayari kwa safari.

Kondoo ya Pasaka 27

Page 28: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Saa sita ya usiku Mungu alipiga wazaliwa wa kwanza wote katika

inchi ya Misri (Kutoka 12:29). Hata mzaliwa wa kwanza ya Farao

aliuawa na malaika ya kuharibu.

Lakini pahali pote Mungu alipoona alama ya damu mlangoni,

alipita juu bila kuharibu. Damu ya kondoo ilipokelewa na Mungu kuwa

malipo ya hukumu. Wale waliojificha na damu waliishi kwa imani.

Walipata uzima kwa njia ya ukombozi.

Kristo ni Mkombozi wetu. Wote ambao wanamwamini, wakipokea

damu yake kuwa ukombozi kwao, wamepata uzima. Wamekombolewa

toka hukumu ya Mungu daima (1 Petro 1:18-19).

28 MIFANO YA KRISTO

Page 29: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MANA, MKATE TOKA MBINGU

(Kutoka 16)

Kisha Mungu alipoondosha Waisraeli katika utumwa wa Misri, wali-

furahi kwanza. Aliwaongoza kuvuka Bahari Nyekundu akiwafanyizia

njia kavu katika maji. Kuonekana kwa Mungu kulikuwa kwa nguzo ya

wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku (Kutoka 13:21). Shekina

iliwaangazia njia ikisimama katikati yao na adui zao.

Jeshi la askari za Misri walijaribu kuwafuata kuwafunga tena kwa

utumwa. Wakaingia juu ya njia kavu baharini, lakini Mungu alirudisha

maji juu yao, wakazama wote (Kutoka 14:26-31). Hivi Mungu alipita

mbele yao kuwaongoza kwa njia ya Kanana.

Lakini jangwani walianza kunungunikia Musa na kumchambua.

Hawakufurahia uhuru wao tena kwa sababu ya majaribu ya safari. Wa-

likumbuka nyama na mkate waliokula kwa Misri, wakashitaki Musa,

wakisema, “Mumetutoa katika jangwa hili kuua kusanyiko hili lote

kwa njaa” (Kutoka 16:3).

Mungu aliwaambia Musa na Haruni jangwani ya kuwa atanyeshea

watoto wa Israeli mkate toka mbingu (Kutoka 16:4). Alitaka kuwapima

kama watashika sheria yake au sivyo na vile wajue ya kuwa Mungu ni

Bwana kweli (sh. 12).

Mungu aliahidi kuwapa mkate toka mbinguni asubui na nyama ya

kutosha mangaribi, washibe (mash. 6-8, 11). Iliwapasa kuokota mana

kila siku asubui, ila siku ya sita wakati watakapopaswa kuokota vipimo

viwili, kimoja kwa siku ile, kimoja kwa sabato (siku ya pumziko la

Waisraeli, ndiyo siku ya saba).

Hivi Mungu alitimiza ahadi yake. Mangaribi kanga wengi waka-

panda, wakafunika kambi. Waisraeli wakawaua wengi (sh. 13).

Asubui, nyuma ya kukauka kwa umande, juu ya udongo wa

jangwa, kulikuwa kitu kidogo cha mviringo, cheupe. Utamu wake

29

Page 30: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

ulikuwa kama asali (sh. 31). Watu walitafuta kukitambua, wakasema

wao kwa wao, “Hiki ni nini?” (mash. 13-15).

Musa akawajibu akisema, “Ni mkate ambao Bwana aliwapa ninyi

kula” (sh.15). Waisraeli wakataja jina lake “mana” (sh.31). Mkate toka

mbingu uliwafikia kuwaponyesha katika njaa. Unaona namna mana

inafanana na Kristo?

Basi, kila mtu alipaswa kuokota kwa yeye mwenyewe kwa kadiri

ya njaa yake na kipimo cha kula kwake (sh.16). Hivi kila mtu alichukua

kipimo cha kufaa kumaliza hitaji lake.

Wengine waliasi, wakiokota siku moja vipimo viwili, wasirudi tena

kuitafuta kesho. Lakini kesho yake walikuta imeoza kabisa. Tena

wengine wakaasi, wakisema, “Faida gani kuokota mara mbili siku ya

sita. Itaoza!” Hivi hawakuokota vipimo viwili namna Mungu alivyo-

waagiza. Basi kesho yake, ndiyo siku ya sabato, mana haikuanguka.

Walibaki na njaa. Lakini wenye kutii waliokota mara mbili siku ya sita,

wakakuta mana yao safi, haikuoza kwa sabato.

Katikati ya safari nzima ya Waisraeli muda wa miaka 40 walikula

mkate kila siku. Mana iliacha kuanguka wakati walipovuka Yorodani,

wakaingia inchini mwa ahadi, wakikula muhindi mpya wa Kanana.

Sasa tufananishe mana ya zamani na Kristo, Mkate wa mbingu.

Zaidi tunapata maelezo haya katika Sura 6 ya Habari Njema ya Yoane.

Pale tunakuta wanafunzi wa Yesu wakati walipokamata mikate mitano

na samaki wadogo wawili kwa mkono wa kijana.

Kwa mwanzo wa Sura 6 ya Yoane Yesu alikulisha wanaume 5000

na zaidi (wanawake na watoto) (mash. 1-13). Lakini toka shairi 22

mpaka 59 tunapata mafundisho mengi juu ya Kristo, Mkate wa

mbingu.

Watu walisema (sh. 31), “Baba zetu walikula mana katika jangwa,

kama ilivyoandikwa: Aliwapa kula mkate toka mbinguni.”

Kwa shairi 32 Yesu aliwaambia, “Siye Musa ambaye aliwapa ninyi

mkate ule toka mbinguni, lakini Baba yangu anawapa ninyi mkate wa

kweli toka mbinguni.”

Tena aliendelea na msemo mwingine kwa shairi 33. “Mkate wa

Mungu ni ule unaoshuka toka mbinguni, na kupa dunia uzima.” Kwa

30 MIFANO YA KRISTO

Page 31: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

shairi 35 aliongeza maneno akisema, “Mimi ni mkate wa uzima, yeye

anayekuja kwangu hatasikia njaa kabisa, naye mwenye kuniamini

hataona kiu kabisa.”

Kweli mana ni sura ya Kristo. Yeye alitoka mbinguni. Alitumwa na

Baba yake, Mungu. Alifika na usafi wote hapa duniani kuwapa watu

uzima.

Watu walinungunikia Yesu wakati aliposema, “Mimi ni mkate

ulioshuka toka mbinguni” (sh. 41). Waliuliza, “Huyu siye Yesu, mwana

wa Yosefu, ambao baba yake na mama yake tunajua? Basi, kwa sababu

gani anasema sasa: Ninashuka toka mbinguni?”

Hawakumtambua kuwa Mwana wa Mungu, si mwana wa Yosefu.

Hawakufahamu yeye ni Mwana wa Mungu tangu milele. Hawakujua

namna alivyoshuka toka mbinguni, “akitwaa namna ya mtumwa,

akakuwa na mfano wa mtu, na akionekana na sura ya mtu, ali-

jinyenyekeza mwenyewe, akakuwa mwenye kutii hata mauti, ndiyo

mauti ya msalaba” (Wafilipi 2:7-8).

Na saburi na mapendo Bwana Yesu aliwaelezea mambo ya siri ya

mkate toka mbinguni. Alisema, “Yeye mwenye kuniamini mimi ana

uzima wa milele. Mimi ni mkate wa uzima. Baba zenu walikula mana

katika jangwa, wakakufa. Huu ni mkate unaoshuka toka mbinguni, ili

mtu apate kuukula, asife. Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka toka

mbinguni; kama mtu akikula mkate huu, atakaa milele; na mkate

ambao nitatoa ni mwili wangu, ambao nitatoa kwa ajili ya uzima wa

dunia” (Yoane 6:47-51).

Mana 31

Page 32: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MWAMBA ULIOPASUKA

(Kutoka 17:1-7)

Sawasawa Waisraeli walivyokuwa na kiu bila maji jangwani, vivyo

hivyo watu duniani leo wanakufa na kiu cha roho, bila tumaini. Mungu

alisaidia Waisraeli kupata maji kuwaponyesha. Sasa Mungu ni tayari

kuwapa maji ya uzima watu wote ambao wanayahitaji.

Waisraeli okoa watu yanapatikana kwa sababu walipata maji safi

toka mwamba uliopasuka. Leo maji ya uzima ni tayari kwa wenye

zambi, wenye kiu kwa roho. Maji ya uzima kuokoa watu yanapatikana

kwa sababu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, alitobolewa wakati alipo-

fungwa juu ya mti wa msalaba. Kwa kupigwa kwake sisi tumepona

(Isaya 53:5).

Mwamba ulipigwa zamani jangwani kusudi maji yatoke, che-

mchemi kumaliza kiu, ni mfano wa Kristo aliyepigwa juu ya msalaba

kwa ajili ya zambi zetu. Alipigwa mara moja tu. Kwa njia ya mauti

yake tunaweza kupata maji ya uzima bila bei (Ufunuo 22:17).

Tuwaze kwanza juu ya mwamba jangwani. Kwa Sura 17 ya Ku-

toka tunapata habari za Waisraeli waliosafiri katika jangwa toka Sinai.

Wakasimama kwa Refidimu. Pale walipiga kambi, wakitandika hema

zao.

Maji ya kunywa yalikosa. Watu wakaanza kugombana na kion-

gozi chao, ndiye Musa, “Utupe maji tupate kunywa” (Kutoka 17:1-2).

Wakaona kiu kabisa, wakanungunikia Musa, wakisema, “Kwa nini

umetupandisha toka Misri, kutuua sisi na wana wetu na nyama zetu

kwa kiu?” (sh.3).

Musa akaomba Yehova Mungu, “Nitafanyia watu hawa nini? Wao

ni karibu kunitupia mawe” (17:4).

Wale watu walikosa tumaini. Walisikia taabu ya kiu, waliogopa

kifo. Watafanya nini? Hivi waligombana na Musa. Mungu alijibu

32

Page 33: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

maombi ya Musa, “Tazama, nitasimama mbele yako pale juu ya

mwamba kwa Horebu; na utapiga mwamba, na maji yatatoka ndani

yake, watu wapate kunywa” (17:6).

Asante. Mungu alisikia kuugua kwa watu, hivi alitunga njia ya

kuwaponyesha. Alichagua mfano wa kufa kwa Kristo na maji ya

wokovu kusaidia Waisraeli.

Musa alipiga mwamba mbele ya wazee wa Israeli (17:6). Maji

yakatoka ndani yake, watu wanakunywa, wakapona. Kristo alipigwa

msalabani kwa gazabu sisi tuliyostahili kupata. Musa alipiga mwamba

mara moja tu.

Nyuma ya miaka mingi Waisraeli walifika tena karibu na mwamba

huu. Wakasikia kiu. Mara hii Mungu aliagiza Musa aseme tu na

mwamba (asiupige). Lakini kwa kasirani juu ya kutokuamini na ku-

tokutii kwa watu, alipiga mwamba na fimbo yake tena. Hivi aliasi

Mungu ambaye alimwagiza aseme tu.

Mfano wa Kristo kupigwa mara moja tu uliharibika. Hivi Mungu

aliazibu Musa, akasema hataingia katika Kanana, inchi ya ahadi. (Soma

Hesabu 20:7-12). Nyuma ya miaka mingi ya kutangatanga kwa Wais-

raeli jangwani, Mungu alipeleka Musa juu ya mlima Pisiga. Toka pale

aliona Kanana mbali, lakini hakupata ruhusa kuingia. Musa alifariki

jangwani. Mungu tu alimzika. (Soma Kumbukumbu la Torati 34:1-8).

Hivi mara ya kwanza mfano ulikuwa sawa. Mwamba ulipigwa

mara moja. Mara ya pili mwamba ulipigwa, lakini haukufaa kwani

ulikuwa sura ya Mwamba wetu Kristo (1 Wakorinto 10:4). Kupigwa

kwa Kristo mara moja kwa msalaba kulifaa kwa kumaliza hasira ya

Mungu juu ya wenye zambi. Waamini wanapata kuondolea kwa zambi

kwa milele. “Kwa kupigwa kwake muliponyeshwa” (1 Petro 2:24).

“Kristo ametolewa mara moja achukue zambi za watu” (Waebra-

nia 9:26,28). Alijitoa mwenyewe kuwa “zabihu moja kwa zambi hata

milele” (Waebrania 10:12). “Kwa toleo moja amekamilisha hata milele

wenye kutakaswa” (Waebrania 10:14). “Basi, pahali maneno haya

yanaposamehewa, hapana toleo tena kwa zambi” (10:18).

Maji yalitoka kwa sababu mwamba ulipigwa katika mapenzi ya

Mungu jangwani. Kristo alipigwa katika mapenzi ya Mungu msala-

bani. Maji ya uzima yanapatikana kama tunda la kufa kwa Kristo.

Mwamba uliopasuka 33

Page 34: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Maji haya ni sura ya Roho Mtakatifu wote wanaoamini Yesu wana-

pata, ndiyo faida ya ukombozi wake.

Bwana Yesu alisema na mwanamke yule wa Samaria, “Kama

ungalijua zawadi ya Mungu, naye ni naniambaye anakuambia, Unipe

maji ya kunywa, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo

hai” (Yoane 4:10). Tena Yesu akamwambia, “Kila mtu . . . anayeku-

nywa maji yale . . . hataona kiu hata milele; lakini maji ambayo ni-

nampa yatakuwa ndani yake kisima cha maji, yanayochemuka hata

uzima wa milele” (Yoane 4:13-14).

Kwa Sura 7 ya Yoane tunasoma maneno haya yaliyotoka kinywani

mwa Yesu: “Mtu akiona kiu aje kwangu, anywe. Yeye anayeamini

mimi, kama maandiko yalivyosema, mito ya maji ya uzima itatoka

tumbo lake. Neno hili alisema juu ya Roho ambaye wale wenye

kuamini watapokea” (7:37-39).

Kwa sisi kuweza kupata maji ya uzima bule kumaliza kiu yetu,

Yesu alipaswa kuteswa msalabani katika moto wa gazabu ya Mungu.

Yeye Mkombozi wetu alitukomboa katika kiu ya Hadeze na ziwa la

moto. Msalabani Yesu alisema, “Nina kiu” (Yoane 19:28).

“Haya, kila mtu anayeona kiu, muje kwa maji, naye asiye na feza;

muje, mununue na mule; ndiyo, muje, mununue mvinyo na maziwa,

pasipo feza na pasipo bei!” (Isaya 55:1).

“Kuja . . . Naye mwenye kiu aje, na yeye anayetaka atwae maji ya

uzima bule” (Ufunuo 22:17). Bwana Yesu anasema, “Mimi nitampa

yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bule” (Ufunuo

21:6).

34 MIFANO YA KRISTO

Page 35: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

NYOKA YA SHABA

(Hesabu 21:4-9)

Tunashangaa kusoma mara kwa mara maneno ya manunguniko ya

Waisraeli. Mungu alitumika na ajabu kwa kuwaondosha katika utumwa

wa Misri. Musa alikuwa kiongozi chao kuwapeleka katika uhuru.

Lakini walitesa Musa tena na tena kwa kumnungunikia.

Kwa wakati wa njaa walisingizia Musa. Mungu alisikia maombi ya

Musa, akawasaidia na mana ya kula. Kwa wakati wa kiu walinungu-

nikia Musa tena. Mungu aliwapa maji kutoka ndani ya mwamba ya ku-

pasuka, wanywe. Kwa kuchambua Musa walinungunikia Mungu

mwenyewe!

Tutasoma sasa katika kitabu cha Hesabu, Sura 21. Tuanze kwa

shairi 4: “Wakasafiri toka mlima Hori kwa njia ya Bahari Nyekundu ili

kuzunguka inchi ya Edomu; na roho za watu zilitiwa mashaka sana

kwa sababu ya njia. Watu wakanungunikia Mungu na Musa: Kwa nini

mumetuleta sisi toka Misri ili tufe katika jangwa? Maana hapana mkate

na hapana maji; na nafsi yetu inachukia chakula hiki bule,” (ndicho

mana, mkate wa mbingu) (Hesabu 21:4-5).

Azabu ya Mungu ilitokea kwao. Mungu alituma nyoka wakali za

moto kuwauma. Watu wengi wakakufa kwa sababu ya sumu ya nyoka

hawa.

Hivi Waisraeli walikuwa pasipo na tumaini. Kwa sababu ya zambi

zao kunungunikia Mungu na Musa, na kubeua mana ambayo alituma

kwao, walikuwa na hatari ya mauti. Wale nyoka wakatambaa huko na

huko katika kambi, tayari kukata watu na sumu.

Watu wakafikia Musa kwa kutubu: “Tumekosa kwa sababu tume-

nungunikia BWANA na wewe; omba BWANA aondoshe nyoka hawa kati

yetu. Musa akaombea watu” (Hesabu 21:7).

35

Page 36: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Mungu aliwaonyesha neema kwa kuwapa njia ya kupona. Walifa-

hamu makosa yao, walikiri zambi mbele ya Mungu na Musa. Hivi

Mungu alitunga njia ya wokovu.

Aliagiza Musa kufanya nyoka ya shaba, aiweke juu ya mti pale

jangwani. Mungu aliahidi ya kuwa mtu ye yote atakayetazama nyoka

ile ya shaba juu ya mti, atapona! (Angalia Hesabu 21:8).

Musa akafanya vile. Akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya

mti. Alipasha watu habari njema. Mtu ye yote aliyeumishwa na nyoka

mkali na kuangalia ile nyoka ya shaba juu ya mti, ataishi. Watu wengi

wakafurahi, wakaangalia nyoka ya shaba kwa imani. Mungu aka-

chunga ahadi yake. Walipona! (Soma Hesabu 21:8-9).

Tunajua nyoka ile ya shaba juu ya mti jangwani ni mfano wa Kristo

juu ya msalaba. Bwana Yesu, yeye mwenyewe, aliifananisha vile.

Fungua Agano Jipya yako pahali Yesu alipozungumuza na Niko-

demo usiku. Utakuta maneno haya kwa Yoane 3:14-15: “Na kama

Musa alivyonyanua nyoka jangwani, vivyo hivyo sharti Mwana wa

watu anyanyuliwe, ili kila mtu akimwamini asipotee, lakini awe na

uzima wa milele.”

Sumu ya nyoka (Shetani) inatupata sisi sote watu wa sasa. Mauti

ni mbele yetu — si mauti ya mwili tu, lakini mauti ya pili, kutengana

na Mungu kwa milele katika ziwa la moto. Hatari ya mauti, mshahara

wa zambi, ni mbele yetu. (Soma Waroma 6:23). Lakini Mungu anataka

tupokee zawadi ya uzima!

Tazama Yesu juu ya msalaba. Yeye anafananishwa kama nyoka

kwa kutuokoa. Yeye ni Mkombozi wetu. “Yeye asiyejua zambi alim-

fanya kuwa zambi kwa ajili yetu ili sisi tuwe haki ya Mungu katika

yeye” (2 Wakorinto 5:21).

Bwana Yesu “hakutenda zambi wala hila haikuonekana kinywani

mwake . . . alichukua zambi zetu katika mwili wake juu ya mti, hata

sisi, tukiwa wafu kwa maneno ya zambi, tuwe hai kwa maneno ya haki;

na kwa kupigwa kwake muliponyeshwa” (1 Petro 2:22-24).

“Kristo alitukomboa kwa laana ya torati, akiwa alifanywa laana

kwa ajili yetu, kama ilivyoandikwa: Amelaaniwa kila mtu anayetu-

ndikwa juu ya mti” (Wagalatia 3:13).

Bwana Yesu alibeba ubaya wetu juu yake, akanyanyuliwa msala-

36 MIFANO YA KRISTO

Page 37: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

bani kama nyoka, kitu kibaya. Laumu yetu na laana yetu zilimfanan-

isha hivi. Mungu alihukumu mwili wetu ndani yake (Waroma 8:3-4).

Mwokozi Yesu alionya watu, “Mutakufa katika zambi zenu; kwa

sababu hamwamini ya kama mimi ndiye, mutakufa katika zambi zenu”

(Yoane 8:24). Yesu aliwaambia: “Wakati mutakaponyanyua Mwana

wa watu, mutafahamu ya kuwa mimi ndiye” (sh.28).

Tena Bwana Yesu alisema katika Yoane 12:32-33: “Nami kama

nikinyanyuliwa juu ya dunia, nitakokota watu wote kwangu. Alisema

maneno haya, akionyesha ni mauti gani ambayo atakufa.”

Musa alihubiri habari njema kwa watu wa zamani walioumizwa

na sumu ya nyoka. “Angalia kwa imani nyoka ya shaba juu ya mti.”

Wakaangalia kwa imani. Wakaponyeshwa!

Leo sisi, watumishi wa Mungu, tunaonyesha Bwana Yesu akikufa

juu ya msalaba, kubeba zambi zetu. Hivi anafanana na nyoka ya shaba.

Tunahubiri Habari Njema: Tubu, tazama Yesu msalabani, kwa

imani. Sumu ya nyoka, hukumu ya zambi, itaondolewa. Uzima uta-

patikana badala ya mauti.

Nyoka ya Shaba 37

Page 38: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

HEMA TAKATIFU

(Kutoka 25:1-9)

Mambo mengi juu ya Kristo yanaonyeshwa katika mifano ina-

yoonekana kwa Hema. Mungu alitaja na Musa, mlimani mwa Sinai,

namna ya kufanya Hema. Alitaja vipimo vyote, namna ya vyuma,

ngozi, vitambaa na vitu vingine vyote. Alituma Musa ashuke mlimani

apashe watu watunge Hema kufuata maagizo ambayo Mungu alimpa

(Kutoka 25:8, 9, 40; 27:8).

Kumbe Hema na vitu vyake vina maana nyingi kueleza juu ya

maisha ya Kristo, kufa kwake na ukuhani wake mbinguni.

Maneno magumu yanayoandikwa katika kitabu cha Waebrania

yanafumbulikana wazi wakati tunapofahamu mifano ya Hema. Hema

ina “mifano ya mambo yaliyo mbinguni” (Waebrania 9:23). Mungu

akusaidie kudumu kutafuta maana hizi za mifano katika Hema, ukue

katika neema na kujua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo (2 Petro

3:18).

Tufahamu ya kuwa Hema ilikuwa nyumba ya nguo na ngozi ili-

yozungukwa na luba kwa kuweka mpaka wa kiwanja. Waisraeli wa-

likaribia Mungu pale. Utakatifu wake ulionekana katika wingu lili-

losimama juu ya Hema.

Hema ilikuwa pahali watu wakosaji walipofikia Mungu na zabihu

kupata ondoleo la zambi. Makuhani waliotajwa na Mungu walimtu-

mikia Hemani siku kwa siku miaka yote waliposafiri jangwani.

Kila mara wakati waliposhika tena njia, Shekina ya Mungu ili-

waongoza. Walipobomoa Hema, Walawi wakabeba vipande vipande.

Waliitandika pahali pengine wakati waliposimama kupanga kwa muda

fulani.

Waisraeli hawakukusanyika ndani ya Hema kama watu wa

makanisa wanavyofanya sasa katika chapelles. Watu walitokea mmoja

mmoja, wakifikia mlangoni mwa Luba, wakitokea na matoleo kumpa

Mungu kama zabihu ya kuteketezwa.

38

Page 39: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MLANGO MMOJA

(Kutoka 27:9-18)

Waisraeli wasafiri jangwani walitoa vitu walivyokuwa navyo kwa ku-

tunga Hema. Zahabu, feza, shaba na nguo ya kitani, na ngozi ndiyo

vitu vyote vilivyohitajiwa. Watu walitoa na roho moja kufanya Hema

kama Mungu alivyowaagiza.

Mafundi wengine walipasua miti ya mshita, wengine walichonga

vyuma. Wanawake walisokota nyuzi kufanya nazo vitambaa, na

kushona mifano juu yao na nyuzi za rangi mbalimbali, kama maagizo

yalivyowaonyesha. Wakati vitu vyote vilipotayarishwa, wakasima-

misha Hema (Kutoka 40).

Kiwanja cha Hema kilikuwa kipimo cha mikono 100 kwa urefu, na

mikono 50 kwa upana. Mkono ni kipimo cha Waisraeli, kutoka kwa

ncha ya vidole kufika kwa kunjo la mkono (coude). Ulikuwa na cen-

timètres 50.

Kuzunguka kiwanja kulikuwa luba ya nguo ya kitani nzuri ya ku-

sokotwa. Urefu juu wa luba ulikuwa mikono mitano. Nguzo 60 zilibeba

nguo ya luba, zenye shaba kwa matako, na vitanzi vya feza.

Luba hii ilikuwa na mlango mmoja tu. Pahali pengine pote mtu

hakuweza kupita luba nyeupe, safi. Lakini kwa mlango wa pekee

atapita.

Nguo ya kitani nyeupe safi, yenye kuzuiza watu, ni sura ya haki

na utakatifu wa Mungu. Mtu hawezi kupita pale. Lakini kwa mlango

atapita na kuingia.

Unafikili mlango huu ni mfano wa nani? Bwana Yesu alisema,

“Mimi ni mlango; kama mtu ataingia kwa mimi, ataokolewa” (Yoane

10:9).

Mtu hawezi kufikia Mungu Mtakatifu leo kwa njia nyingine ila

kwa Yesu mwenyewe. Yeye alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na

uzima: mtu hakuji kwa Baba, ila kwa mimi” (Yoane 14:6).

39

Page 40: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Mlango wa luba ya Hema ni mfano wa Yesu. Upana wa mlango

ulikuwa mikono 20. Tandiko la mlango lilikuwa nguo za rangi ya

samawi (bleu) na zambarau (pourpre) na nyekundu na kitani nzuri

yenye kusokotwa. Rangi hizi zinatukumbusha juu ya mbingu pahali

Yesu alipotoka, na ya kuwa yeye ni Mfalme kabisa. Nyekundu

inaonyesha damu yake, na kitani safi, utakatifu wake. (Tazama Kutoka

27:16-17 na Kutoka 38:9-20).

MAZABAHU YA SHABA

(Kutoka 27:1-8; 38:1-7)

Mara moja ndani ya mlango wa kiwanja cha Hema kulikuwa ma zabahu

ya sadaka. Ilisimama mlangoni kama zamu. Mtu hawezi kufika mbele

ya Mungu ila damu ya mkombozi imwangike.

Mazabahu hii ilikuwa mraba ndiyo kusema vipimo sawa pande

zote. Urefu mikono mitano, upana mikono mitano. Urefu wake juu

mikono mitatu. Ilifanywa na mbao za mti wa mshita, usiooza, kufu-

nikwa pande zote na chuma cha shaba kisichoweza kuyeyuka katika

moto.

Mazabahu ikiwa mraba inaonyesha ya kama mtu ye yote toka

pande zote duniani ataweza kufika namna moja bila tofauti kupata faida

ya mkombozi. Mti wa mshita unaonyesha mwili wa Yesu wa kimtu,

bila kosa, usioweza kuoza (1 Petro 2:22; Matendo 13:35) .

Shaba ina maana ya hukumu, katika Biblia. Vilevile hapa tunaona

umungu wa Yesu (shaba) na umtu wa Yesu (mti wa mshita). Mazabahu

ni sura ya Kristo aliyevumilia hukumu ya Mungu na moto wa gazabu

yake kwa ajili yetu. Yesu ni mazabahu (Waebrania 13:10), na vilevile

sadaka juu ya mazabahu ni Kristo. Hivi kwa pahali pamoja kuna mi-

fano miwili juu ya Mwokozi wetu. Kristo mwenyewe alitakasa zabihu

iliyotolewa juu ya mazabahu. Kwa Matayo 23:19 tunasoma, “Maza-

bahu inayotakasa sadaka.”

Mwenye zambi aliweza kufikisha nyama safi (kama ndume ya

ngombe au kondoo au mbuzi, hata hua). Aliweka mkono wake juu ya

40 MIFANO YA KRISTO

Page 41: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

kichwa cha nyama kuonyesha ya kuwa nyama huyu amekuwa mko-

mbozi wake. Nyama alichinjwa pale, damu yake kuvuja kando ya ma-

zabahu. Vipande vya nyama kuhani alivyoweka juu ya mazabahu,

vikiteketezwa kwa moto. Hivi mtu yule alipokelewa na Mungu, zambi

zake zilifunikwa.

Kuzidi sana zabihu ya Kristo ni sadaka ya kupendeza Mungu. Kwa

toleo lake amepatia usamehe wa zambi mtu ye yote ambaye

anamwamini, na salama na Mungu.

Bwana Yesu alijitoa kukubali mapenzi ya Baba Mungu, kuwa mkom-

bozi wetu. Mara moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana aondoe

zambi kwa kujitoa mwenyewe (Waebrania 9:26; Yoane 10:17-18).

Matoleo mbalimbali yalitolewa pale juu ya mazabahu. Yanaonye-

sha mifano ya Kristo. Katika kitabu cha Walawi tunapata maagizo juu

ya sadaka hizi namna namna. Kama ukisoma sura hizi, utashangaa juu

ya maana ya damani juu ya Kristo pale.

Tukamate sadaka mbili kwa kukuonyesha. Kwa Walawi 4 tunap-

ata “Sadaka kwa zambi.” Soma mashairi 1-12. Uisawanishe na Kristo

aliyebeba zambi zetu juu yake kwa ukombozi wa hukumu yetu. “Yeye

asiyejua zambi alimfanya kuwa zambi kwa ajili yetu ili sisi tuwe haki

ya Mungu katika yeye” (2 Wakorinto 5:21). Kristo alikuwa sadaka ya

zambi kwa sisi.

Tuangalie sasa Walawi, Sura 1. Soma juu ya sadaka ya kuteke-

tezwa. Anza kwa shairi 3, soma mpaka shairi 13. Toleo hili ni moja

katika matoleo yenye harufu ya kupendeza Mungu (mash. 9, 12). Kwa

zabihu hii ya kuteketezwa (ndiyo kuchomwa, kuungua pia) tumepata

mfano wa Yesu kwa usafi wake akijitoa mbele ya Mungu kuwa sadaka

ya kumpendeza, kufikia pua ya Mungu kama manukato matamu.

Kwa Kristo, kama katika nyama ya sadaka kwa zambi, tunapata

ukombozi toka hukumu ya Mungu kwa ajili ya zambi (Waefeso 1:7).

Kwa Kristo, kama katika nyama ya zabihu ya kuteketezwa, tuna-

pata kukubaliwa na Mungu kwa ajili ya uzuri wa Kristo na kutii kwake.

Nyama ya zabihu ya kuteketezwa ilitolewa “ikubaliwe kwa ajili yake

kwa kumfanyia upatanisho” (Walawi 1:4). Sisi tunakubaliwa kwa

upatanisho na Mungu kwa njia ya kufa kwake badala yetu.

Mazabahu ya shaba 41

Page 42: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

BIRIKA LA SHABA

(Kutoka 30:17-21)

Mazabahu ya shaba ilikuwa ndani ya mlango wa luba ya kiwanja cha

Hema. Pale sadaka zilitolewa, damu ilimwangika, zabihu iliteketezwa

kwa moto.

Mbele kidogo, ndani, katikati ya mazabahu na Hema Takatifu

yenyewe, kulikuwa birika la shaba, kama sahani kubwa ya chuma pahali

makuhani walipopaswa kunawa mikono na miguu (Kutoka 30:17-21).

Hivi kulikuwa vitu viwili tu kiwanjani, vyote vya shaba. Mazabahu

ilichanganyisha shaba na mti wa mshita. Maana ya shaba ni umungu na

utakatifu wa Kristo, na mti wa mshita ni umtu wake (Kutoka 40:30-32).

Kisha kuhani alipoingia kwa mlango wa pekee wa luba, alipita kwa

mazabahu ya sadaka. Halafu aliendelea mbele kwendea Hema.

Lakini siku kwa siku ilimpasa kunawa mikono na miguu kwa

birika la shaba mbele ya kuingia ndani ya Hema kutumikia Mungu.

Alihitaji maji katika birika kujinawa kuondosha uchafu aliopata kwa

kutembea udongoni, na kukamatakamata vitu mikononi mwake.

Wakati Haruni na wana wake walipowekwa kuwa makuhani mara

ya kwanza, Musa aliwapeleka kwa mlango wa Hema, akawasafisha

mwilini mwote pia na maji safi. Hawakuhitaji kuoga kwa kutimiza she-

ria tena. (Ndiyo, hemani zao, pahali walipopanga, walioga maji kama

watu wote, lakini si kwa sheria ya utumishi wao wa ukuhani). Mara

moja ilitosha. Toka pale, iliwapasa kunawa kila siku kwa birika.

Vivyo hivyo kwa makuhani wa sasa. Waamini wote wanapata

ruhusa ya ukuhani (1 Petro 2:5,9). Tuna ruhusa kufikia Mungu.

Tukipata faida ya sadaka ya Kristo msalabani kwa ajili yetu, tume-

okolewa kwa milele. Tunatakaswa daima kwa zabihu moja. Soma Wa-

ebrania 10:14, “Kwa toleo moja amekamilisha hata milele wenye

kutakaswa.” Tumepata usamehe, hatuhitaji toleo tena (Waebrania 10:18).

42

Page 43: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Wakati Petro alipoona Yesu akinawa miguu ya wafuata wenzake,

na Yesu alitaka kunawa yake vilevile, Petro alikataa. Bwana Yesu

alimwambia, “Kama nisipokunawa wewe, huna shirika pamoja nami”

(Yoane 13:8). Hivi Petro aliomba Yesu amwogeshe mwili mzima.

Lakini Yesu alimwambia, “Yeye aliyeoga hahitaji ila kunawa miguu

yake tu, lakini yeye ni safi kabisa” (Yoane 13:10).

Mkristo ametakaswa mbele ya Mungu siku alipoamini Yesu. Damu

yake inamsafisha. Sasa yeye ni kuhani kutoa zabihu ya roho za kupe-

ndeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo (1 Petro 2:5). Lakini hawezi ku-

fika mbele ya Mungu na zambi za mwenendo. Sharti anawe mbele ya

kufika kwake.

Zamani kuhani aliyetumikia Mungu katika Hema jangwani ali-

kwenda kwa birika la shaba kunawa. Birika la shaba linafanana na

Yesu. Sisi makuhani tunahitaji kufika mbele yake kila siku, kukiri

zambi zetu na kuomba kusafishwa.

Yesu ni NENO (Yoane 1). Tunafika kwake atusafishe kwa Neno

lake la haki, ndilo Maandiko Matakatifu. Maji katika birika zamani

yanafanana na Neno la Mungu. Bwana Yesu aliomba Baba Mungu

(Yoane 17:17), “Uwatakase kwa kweli; neno lako ni kweli.”

Tunahitaji kusafishwa kila siku na maji ya Neno la Mungu. “Kristo

alivyopenda kanisa, na kujitoa mwenyewe kwa ajili yake; apate kuli-

takasa, akiwa amelisafisha kwa maji katika neno” (Waefeso 5:25-26).

Mtu anayeamini Bwana Yesu anasafishwa na zambi. Paulo

aliandikia Wakorinto, “Wengine kwenu mulikuwa hivi; lakini

mulioshwa, lakini mulitakaswa, lakini mulihesabiwa kuwa na haki

katika jina la Bwana Yesu, na katika Roho ya Mungu wetu” (1 Wako-

rinto 6:11). Hii ni kuoshwa kwa wokovu.

Nyuma Paulo aliwaandikia maneno mengine juu ya kusafishwa

kwa kila siku, “Tujisafishe kwa uchafu wote wa mwili na wa roho, tuk-

itimiza utakatifu katika woga wa Mungu (2 Wakorinto 7:1).

Mkristo anayechafuka na zambi ya dunia, sharti afike kwa Bwana

Yesu ndiye Birika letu, kukiri na kutubu. “Kama tukisema kwamba

hatuna zambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli si ndani yetu.

Tukikiri zambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee

zambi zetu, na kutusafisha na uzalimu wote (1 Yoane 1:8-9).

Birika la shaba 43

Page 44: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kuhani akiingia mbele ya Mungu kutoa sifa, asiyesafishwa na

zambi zake za mwenendo, ana hatari ya azabu ya Mungu.

Fikili maneno ya watoto wa Haruni, Nadabu na Abihu. Wao wa-

likuwa makuhani lakini walifika mbele ya Mungu kutoa uvumba na

kuuchoma na moto usiofaa. Moto ulitoka kwa Bwana, ukawakula,

wakakufa mbele ya Bwana (Walawi 10:1-2).

Hivi, “Mtu ajihukumu mwenyewe ... kwa sababu hii wengi kwenu

ni zaifu na wagonjwa, na wengi wamelala. Lakini kama tungejihukumu

sisi wenyewe, tusingehukumiwa” (1 Wakorinto 11:28, 30-32) .

Birika la shaba

44 MIFANO YA KRISTO

Page 45: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

KINARA CHA ZAHABU

(Kutoka 25:31-40)

Hema ya kusanyiko ilikuwa na vyumba viwili: Pahali Patakatifu na

Pahali Patakatifu pa Patakatifu. Hivi chumba cha pill kilikuwa patakat-

ifu zaidi sana. Pale wingu wa utukufu wa Mungu ulikawa juu ya kiti

cha neema.

Katika chumba cha kwanza, ndicho Pahali Patakatifu, kulikuwa

vitu vitatu: kinara cha zahabu, meza ya mkate wa onyesho na maz-

abahu ya uvumba. Meza na mazabahu zilifanywa kwa mti wa mshita,

zikifunikwa na zahabu. Lakini kinara kilifanywa na zahabu safi tike.

Fundi hakuyeyusha zahabu wakati alipofanya kinara, lakini aliipi-

gapiga na nguvu iwe chuma kimoja.

Tuwaze kwanza juu ya kinara cha zahabu. Urefu wake haujulikani,

lakini kilikuwa kitu cha damani, kizuri sana. Nguzo ya kati pamoja na

matawi matatu ngambo moja na matatu ngambo nyingine yalifanya

matawi saba (hesabu kamilifu). Nguzo na matawi yake yalichongwa na

zahabu safi kwa fundi aliyefuatua maua ya mbegu ya lozi. Nguzo na

matawi yalibeba taa saba za zahabu.

Kuhani aliingia kila siku, nyuma ya kunawa inje katika birika,

kutengeneza taa hizi saba, kuondosha makaa juu ya vitambi na kujaza

mabakuli na mafuta ya zeituni kama Mungu alivyowaagiza. Hivi taa

ziliwaka daima (Walawi 24:2, 4). Maneno haya tunapata katika kitabu

cha Kutoka 25:31-40 na vilevile kwa Sura 37:17-24.

Nuru ya inje haikuingia ndani ya Pahali Patakatifu. Taa saba zili-

waka zikiangaza nuru juu ya kinara kuonyesha uzuri wake (Kutoka

25:37). Kinara kilimetameta katika usafi wake wa zahabu ya ku-

chongwa.

Sasa tutafute maana ya kinara na taa zake. Kinara ni mfano wa

Kristo. Zahabu inaonyesha umungu wake. Usafi wa zahabu unashuhu-

dia usafi wa moyo wa Kristo.

45

Page 46: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kristo alipigwa, aliteswa kama chuma cha kinara kilivyopigwa na

kilivyokatwa wakati wa kukichonga (Soma Isaya 53:5).

Kristo ni nuru ya ulimwengu, akifika kuangazia watu katika giza

la dunia (Yoane 1:4-5; 8:12; 9:5; 12:46).

Taa saba ni sura ya makanisa katika umoja wa Kristo duniani pote.

Kuwaka kwa kuangaza na nuru sasa ni kazi ya makanisa (Ufunuo 1:20;

Waefeso 5:8). Kama taa zilivyowaka kuonyesha uzuri wa kinara, vivyo

hivyo makanisa yanashuhudia uzuri wa Kristo na neema yake. Petro al-

ituambia ya kuwa kazi yetu ni kutangaza uzuri wake aliyetuita toka

giza tuingie katika nuru yake ya ajabu (1 Petro 2:9).

Moto wa ushuhuda unawaka na mafuta ya Roho Mtakatifu. Mafuta

ndani ya mabakuli ya taa za kinara ni mfano wa Roho Mtakatifu. Roho

Mtakatifu anafurahi kuonyesha utukufu wa Kristo. (Soma Yoane

16:13-14).

Hesabu ya saba katika Biblia ni hesabu ya ukamilifu. Tunaona

hesabu hii kwa Ufunuo 4:5 juu ya Roho Mtakatifu na ukamilifu wa

ushuhuda wake. Kwa Ufunuo 1:10-13 tunaona Yesu katikati ya

makanisa saba, akipitisha mawazo yake kwao. Makanisa saba ni se-

hemu sehemu ya Kanisa la dunia pote.

Maua na mbegu ya lozi zilizochongwa juu ya kinara zinaonyesha

matunda toka katika mauti na maisha ya Kristo. Yeye ni mwenye kuzaa

tunda (Yoane 12:24).

Kama sisi tukitaka kuzaa tunda kwa Yesu, tujitoe kwake, uzima

wake utumike ndani yetu. Soma Yoane 15 juu ya mzabibu na matawi

yake. Tuko mwili mmoja na yeye. Kukaa kwake kunatupa uwezo kuzaa

tunda la Roho.

Roho Mtakatifu ndani ya Mkristo analeta mafuta kwa taa kuwaka.

Lakini kama makaa ya zambi yakifungana juu ya kitambi, inafaa

kuhani aondoshe makaa, mafuta ya Roho yatelemke na usafi hata moto

wa ushuhuda uwake vizuri bila zuizo.

46 MIFANO YA KRISTO

Page 47: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MEZA YA MKATE WA ONYESHO

(Kutoka 25:23-30; Walawi 24:5-9)

Meza hii inatuonyesha mfano wa Kristo na watu wake katika ushirika.

Urefu wake ulikuwa mikono miwili. Upana wake ulikuwa mkono

mmoja. Kusimama kwake juu ulikuwa mkono mmoja na nusu.

Mafundi walitumia mti wa mshita kufanya meza hii. Juu yake

pande zote walifunika mbao na zahabu. Taji ya zahabu iliizunguka pale

juu. Pete zilikuwa kwa pembe zake ine, pahali pa kuingiza magongo.

Magongo ya mshita yalifunikwa vilevile na zahabu. Wakati wa kusafiri

walibeba meza na magongo haya.

Meza ilikuwa pamoja na kinara cha zahabu ndani ya chumba cha

Hema kilichoitwa “Pahali Patakatifu.” Kila sabato kuhani ataweka

mikate kumi na miwili juu ya meza, kwa mistari miwili, sita, sita.

Wakati wa kuondosha mikate ya mbele, makuhani waliikula.

Juu ya mikate mezani kuhani alimimia marashi, ndiyo ubani safi,

kwa manukato. Hivi kwa juma moja zima mikate ilishinda pale kwa

meza kunuka na harufu tamu mbele ya Mungu.

Makabila 12 ya Israeli yalionyeshwa mbele ya Mungu ndani ya

mkate wa onyesho. Ni kama vilevile kuhani mkubwa alivyobeba ma-

jina yao mbele ya Mungu juu ya kifua chake (Kutoka 28:15, 21) na

kwa mabega yake kwa efodi (Kutoka 28:6,12). Wakati kuhani mkubwa

alipoingia, alipeleka majina ya makabila ya Israeli mbele ya Mungu.

Wakati mwingine taifa la Israeli lilitengana kuwa sehemu mbili

mbalimbali. Sehemu moja ilikuwa na makabila mawili. Sehemu

nyingine ilikuwa na makabila kumi. Lakini hata hivi, wakati wote kwa

meza mikate ilikuwa 12. Vilevile Mungu hakuita mikate 12 “mikate.”

Aliiita “mkate wa onyesho,” kutangaza umoja wao.

Mikate 12 ilikuwa alama ya watu wa Mungu pia. Sisi sasa tunap-

ata maana nzuri sana katika meza ya zahabu na mkate wa onyesho.

47

Page 48: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Kwa mfano, tunafahamu Yesu ni meza ya zahabu anayebeba watu

wake wote mbele ya Mungu daima. Kwa umoja anawaonyesha na

manukato matamu mbele ya Baba yake.

Vilevile analinda watu wake kwa uwezo wake, mkononi mwake.

Hawawezi kuponyoka kamwe. Ni kama meza ilivyochunga mkate kwa

taji ya zahabu iliyoizunguka pande zote.

Mti wa mshita meza iliyofanywa nao unafanana na umtu wa Kristo

ambaye alitukufilia msalabani. Zahabu inatangaza umungu wake na

utukufu wake. Taji ya zahabu iliyozunguka meza inaonyesha utawala

wake. Yeye ni Mfalme wa wafalme. Atatawala duniani pote.

Mkate ni watu wake. Meza na mkate juu yake zinafanana na

Bwana Yesu katika ushirika wake na watu wake. Anawaonyesha mbele

ya Mungu kama meza ilivyobeba mkate mbele yake zamani (Waroma

8:34).

Tunaweza kusawanisha mkate vilevile na Yesu mwenyewe. Yeye

ni mkate aliyetoka mbinguni, kuwapa watu uzima. Yeye alikufa kama

punza ya ngano (Yoane 12:24). Alisagwa kama mbegu ya ngano kuwa

unga wa kufanya mkate. Tena Bwana Yesu aliwekwa kwa moto katika

tanuru ya gazabu ya Mungu hata sisi tuwe mkate kutoka ndani ya

mateso yake, ndani yake mwenyewe. Anatuonyesha mbele ya Baba

yake kwa utamu, tunda la mateso na mauti yake.

48 MIFANO YA KRISTO

Meza yaMkate wa Onyesho

Page 49: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

MAZABAHU YA KUCHOMA UVUMBA

(Kutoka 30:1-10)

Vyumba viwili vya Hema vilikuwa na kitambaa kubwa kuvigawa. Ki-

tambaa hiki kiliitwa “pazia.”

Vitu viwili vilikuwa chumbani cha kwanza. Vilikuwa kinara cha

zahabu na meza ya mkate wa onyesho iliyofunikwa po pote kwa za-

habu.

Kitu cha tatu kilichokuwa ndani ya chumba cha kwanza kiliitwa

“mazabahu ya kuchoma uvumba.” Mazabahu hii haikuwa pahali pa

kutoa nyama ya sadaka. Ilikuwa mazabahu pahali kuhani alipochoma

uvumba mbele ya Mungu ndio manukato ya kuteketezwa.

Mazabahu hii ilifanywa na mti wa mshita na kufunikwa pahali po

pote na zahabu. Soma Kutoka 30:1-10. Urefu wake ulikuwa mkono

mmoja, upana wake vivyo hivyo kwani ilikuwa mraba. Kusimama

kwake juu kulikuwa mikono miwili. Ilikuwa na pembe zake za zahabu

na taji ambayo iliizunguka. Taji vilevile ilifanywa na zahabu.

Mazabahu ya kuchoma uvumba iliwekwa mbele ya pazia iliyo-

gawa vyumba viwili vya Hema. Kila mangaribi wakati kuhani alipo-

tokea kuwasha taa za kinara, aliongeza makaa kwa mazabahu hii ya

zahabu. Makaa yalitoka kwa mazabahu ya shaba ya sadaka ya nyama

kiwanjani. Hivi moto uliwaka na uvumba mtamu juu mazabahu ya za-

habu daima.

Kila mwaka mara moja kuhani mkubwa alikamata damu ya zabihu

toka mazabahu ya shaba kiwanjani kuifikisha ndani ya Pahali Pataka-

tifu. Pale alinyunyiza pembe za mazabahu ya kuchoma uvumba na

damu, kufanya upatanisho na Mungu. Kama mwabudu ametakaswa na

damu aliweza kutoa sifa ya kufaa mbele ya Mungu. Shukrani isiyo-

takaswa haiwezi kupokelewa na Mungu.

Mazabahu ya kuchoma uvumba inatukumbusha kazi ya Kristo

49

Page 50: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

sasa mbinguni kwa ajili ya watu wake. Yesu anatuombea mbele ya

Mungu (Waebrania 7:25; 9:24).

Kwa yeye tu tunaweza kutoa sifa zetu. Yeye ni mazabahu yetu ya

zahabu. Tulifahamu mbele namna mti wa mshita ulivyoonyesha utu

wa Kristo na zahabu ilivyoonyesha umungu wake. Yeye ni Mwana wa

mtu na Mwana wa Mungu. Ni Yesu, mtu, ambaye anatuombea mbi-

nguni (Waebrania 7:25).

Sisi Wakristo tunatoa shukrani na kuabudu mbele ya Mungu kwa

njia ya Yesu. Soma Waebrania 13:15, “Basi, kwa njia yake, tumpe

Mungu zabihu ya sifu siku zote, ndiyo tunda la midomo inayokiri jina

lake.”

Kwa Ufunuo 8:3-4 tunasoma juu ya malaika aliyesimama mbele ya

mazabahu ya kuchoma uvumba. Malaika huyu ni Yesu. Sikia neno hili

juu yake, “Malaika mwingine alikuja, akasimama mbele ya mazabahu,

mwenye chungu cha zahabu; akapewa uvumba mwingi, ili autie

pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya mazabahu ya zahabu

iliyo mbele ya kiti cha ufalme. Na moshi wa ule uvumba ukapanda

mbele ya Mungu pamoja na maombi ya watakatifu toka mkono wa

malaika.”

Asante kwa Mungu. Bwana Yesu sasa, kuhani letu mkubwa,

anaongeza uvumba wa marashi yake juu ya maombi na shukrani zetu.

Hivi zote zinapanda pamoja kuwa manukato matamu kwa moto ya

Roho Mtakatifu kufurahisha Mungu.

Wakristo wote wana ruhusa ya ukuhani mbele ya Mungu. Petro

aliandika, “Ninyi vilevile, kama mawe yaliyo hai, mumejengwa muwe

nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, kutoa zabihu za Roho, za kupe-

ndeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo” (1 Petro 2:5). Kwa yeye, kuhani

letu mkubwa, tunatoa zabihu za sifa mbele ya Mungu.

Lakini makaa ya kuchoma uvumba wa sifa yawe ya Roho Mtaka-

tifu, kwa moto wa msalaba na damu ya Sadaka yetu. Mtu asilete sifa toka

moto mgeni. Soma azabu juu ya wana wa Haruni (Walawi 10:1-2).

50 MIFANO YA KRISTO

Page 51: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

PAZIA, SANDUKU YA AGANO NA

KITI CHA REHEMA

(Kutoka 26:31-32; 25:10-22; 37:1-9)

Pazia liligawa vyumba katika Hema. Lilifanywa kuwa kitambaa cha

kitani nzuri ya kusokotwa. Nyuzi za rangi ya samawi, zambarau na

nyekundu zilishonwa kuonyesha sura ya makerubi (Kutoka 26:31-32).

Makuhani wo wote hawakuwa na ruhusa kuingia kupita kwa

chumba cha ndani ndicho “Pahali Patakatifu pa patakatifu,” ila kuhani

mkubwa mara moja kila mwaka kwa siku ya malipizo. Yeye alipaswa

kubeba damu kunyunyiza juu ya kiti cha rehema kwa ajili yake

mwenyewe na kwa zambi za Israeli wote (Waebrania 9:6-7).

Miaka mingi nyuma, wakati Waisraeli walipoishi katika inchi ya

Kanana, walikomboa Hema na hekalu, kwani safari yao jangwani ili-

kwisha. Pazia liligawa vyumba vya hekalu namna lilivyogawa vyumba

vya Hema. Watu walizuizwa kufika ndani kabisa, ila kuhani mkubwa.

Lakini wakati Yesu alipokufa msalabani, pazia la hekalu lilipa-

suliwa toka juu fika chini. Njia ya kufikia Mungu kwa kila mwamini

imefunguliwa wazi sasa. Mazuizo yaliondoshwa wakati Mwokozi Yesu

alipotobolewa.

“Tuna uhodari wa kuingia Pahali Patakatifu kwa damu ya Yesu,

njia ile aliyoanza kwa ajili yetu, mpya, na hai, katika pazia, ndio mwili

wake; na tukiwa na kuhani mkubwa juu ya nyumba ya Mungu; tukari-

bie kwa moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, mioyo yetu ikikwisha

kunyunyiziwa kwa kuacha zamiri mbaya, na miili yetu kuoshwa kwa

maji safi (Waebrania 10:19-22).

Vivuli vya zamani vinatimizwa katika haki ya mbingu.

Turudi sasa kwa maneno ya Hema jangwani. Ndani ya chumba cha

pili (cha ndani, nyuma ya pazia) kulikuwa sanduku ya agano na juu

yake kiti cha rehema. Tunapata habari zao katika Kutoka 25:10-22.

51

Page 52: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Sanduku ilifanywa na mti wa mshita kufunikwa ndani na inje na

zahabu safi. Urefu wake juu ulikuwa mikono mmoja na nusu. Ilikuwa

na pete ine za zahabu kwa kuibeba wakati wa kuhama, na magongo ya

mshita yaliyofunikwa na zahabu.

Kifuniko cha sanduku kilikuwa ya zahabu tike waliyopigapiga ku-

tunga makerubi wawili wakitazamana. Katikati yao ni pahali kuhani

mkubwa alipoweka damu toka sadaka inje juu ya mazabahu ya shaba.

Kifuniko hiki kiliitwa “kiti cha rehema.”

Ndani ya sanduku kulikuwa vitu vitatu. Tusome kwa Waebrania

9:3-4, “Nyuma ya pazia la pili ilikuwa hema iliyoitwa Pahali Patakat-

ifu pa patakatifu, yenye chetezo cha zahabu na sanduku ya agano iliy-

ofunikwa na zahabu pande zote, na ndani yake kulikuwa kopo la

zahabu lenye mana, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya

agano; na juu yake makerubi ya utukufu, yakitia kivuli juu ya kiti cha

rehema.”

Kopo la zahabu (Kutoka 16:33-34) lilichunga kipimo cha mana

ambayo Waisraeli walikula jangwani. Haikuoza. Ilikuwa ushuhuda wa

uaminifu wa Mungu ambaye aliwakulisha jangwani. Kwa sisi mana

hii ni mfano wa Kristo, mkate wa mbingu (Yoane 6:31-35, 50-51).

Fimbo ya Haruni iliyochipuka (Hesabu 17:5-11) iliwekwa katika

sanduku kushuhudia zambi za watu (Hesabu, Sura 16 na 17). Mungu

aliazibu waasi. Fimbo 12 zisizo na uzima ziliwekwa zamani mangaribi

Mungu aonyeshe ni nani atakayemchagua kuwa kuhani lake. Asubui

fimbo ya Haruni ilionekana pekee kuwa na uzima, kuchipuka na kuzaa

maua na matunda ya lozi. Kwa sisi tunaona kwa fimbo ya kuchipuka

mfano wa Kristo katika mauti yake tena kuonekana na uzima, mwenye

kuzaa matunda katika ufufuko wake (Yoane 12:24).

Vibao vya sheria vilikuwa katika sanduku kwa Hema na kwa hekalu

(mana na fimbo hazikuwa kwa hekalu). Vibao vya sheria vilibaki kuonye-

sha ya kuwa sheria ya Mungu inadumu daima. Mwokozi Yesu hakufika

kuharibu sheria, lakini kuitimiza (Matayo 5:17).

Kiti cha rehema cha zahabu safi kinaonyesha namna mtu ataka-

vyoweza kukutana na Mungu. Damu ya sadaka inanyunyizwa juu ya

kiti cha rehema. Ushirika katikati ya Mungu na watu unawezekana kwa

ajili ya damu ya Yesu kumwangika kwa ajili yetu, kutuliza gazabu ya

52 MIFANO YA KRISTO

Page 53: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Mungu.

Makerubi ya zahabu juu ya kiti cha rehema kwa sanduku ya agano

hayakuwa na mapanga ya hukumu kama wale waliowekwa kulinda

njia ya shamba la Edeni wakati Adamu na Hawa walipokosa na ku-

fukuzwa.

Makerubi hapa yanakunja mabawa yao kimya, yakitazamana na

kuangalia damu juu ya kiti cha rehema. Sheria iliyovunjwa kwa

mikono ya watu sasa imewekwa chini ya damu ya ukombozi, ndiyo

damu ya zabihu. Hivi salama na amani zinapatikana kwa wenye zambi.

Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema

Pazia 53

Page 54: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

KUHANI MKUBWA NA MAVAZI MATAKATIFU

(Kutoka 28:1-43; 39:1-31)

Kuhani mkubwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Haruni, ndugu yake

Musa. Yeye alikuwa mtu wa kabila la Lawi. Watoto wake walitakaswa

kuwa makuhani.

Kuhani mkubwa wa zamani ni mfano wa Kristo na utumishi wake

wa sasa. Ukuhani wa makuhani ya zamani ulibadilika. Kuhani alikufa,

mwingine alimkomboa kwa kazi. Lakini ukuhani wa Kristo unapita

ule wa Walawi, namna ya Haruni, kwani Kristo anaishi kwa milele,

haubadiliki kamwe. Anadumu kuombea watu wake mbele ya Mungu

daima (Waebrania 7:21-27) .

Ukuhani wa Kristo ni mzuri kupita ule wa Haruni. Kristo alitoka

kabila la Yuda, ndilo la wafalme. Kweli yeye ni mfalme. Lakini namna

gani ataweza kuwa kuhani asiye wa kabila la Lawi? Yeye ni kuhani

namna ya Melkisedeki aliyekuwa kuhani la Mungu aliye juu na mfalme

wa Salemi (Mwanzo 14:18-20).

Melkisedeki alikuwa mtu wa ajabu. Namna ya kuzaliwa kwake

haijulikani. Anafanana na Kristo aliyezaliwa kwa ajabu: Baba yake

Mungu, mama yake bikira.

Abrahamu, baba yake Isaka aliyezaa Yakobo baba ya Lawi, ali-

jinyenyekeza mbele ya kuhani Melkisedeki, akitoa zaka ya moja ndani

ya kumi ya nyara zote alizopata ndani ya vita. Hivi Abrahamu aliinama

mbele ya mkubwa. Lawi alitoka kwa uzazi wa Abrahamu. Hivi ni kama

Lawi alijinyenyekeza mbele ya Melkisedeki. Maana: ukuhani wa Lawi

(Haruni) haufiki kwa ukubwa wa ukuhani wa Melkisedeki. Kristo ana-

fuata Melkisedeki katika ukuhani wa juu kupita. (Soma Waebrania

6:20; 7:1-28).

Mara moja kila mwaka kuhani mkubwa aliingia kupita pazia ndani

ya chumba cha pili ndicho Pahali Patakatifu pa Patakatifu. Alipeleka

damu toka mazabahu ya sadaka kunyunyiza juu ya kiti cha rehema.

54

Page 55: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Yesu, Kuhani letu mkubwa anayeishi milele, aliingia mara moja

kwa Pahali Patakatifu na damu yake mwenyewe. (Soma Waebrania

9:11-15). Hahitaji kujitoa mara nyingi kama kuhani la zamani, lakini

kwa toleo lake mara moja ametakasa na kukamilisha watu wake (Wa-

ebrania 9:23-28; 10:14).

Itakuwa faida kusoma Waebrania 4:14-16 na Sura 5, 7, 8, 9, 10.

Pale utapata mambo ya kutimiza mifano ya Hema ya jangwa, na ma-

toleo na kazi ya kuhani mkubwa. Utafahamu maneno ya Kristo zaidi

kupita kama ukiwaza juu ya mifano katika Agano la Kale, na kusoma

maana katika Agano Jipya.

Makuhani ya zamani walitumikia Hema ya dunia lakini Kuhani

letu mkubwa anatumikia mbinguni kabisa. Kwa Hema ya zamani tu-

napata kivuli cha maneno ya kweli mbinguni. Sadaka za Israeli zamani

hazikuweza kukamilisha wenye kukaribia Mungu wala kumpendeza.

Lakini zabihu ya Kristo inafaa. (Soma Waebrania 10:14, 19-22).

Mavazi ya kuhani mkubwa wa zamani yana maana kwa kufana-

nishwa na utumishi wa Kristo katika ukuhani wake. Alivaa nini wakati

alipokaribia Mungu?

Kwanza, kanzu yenye mkono, nyeupe ya kitani nzuri na

mirabaraba (kazi ya mshonaji). Nyeupe kuonyesha usafi wa Yesu

katika utu wake (Kutoka 28:4). Juu ya kanzu alivaa joho (koti) mfupi

bila mikono ya rangi ya samawi (kama mbinguni). Hili vazi lilisokotwa

kwa umoja. Kristo ni mwenyeji wa mbingu. Pindo za joho chini

zilibeba mifano ya matunda ya makomanga, yenye rangi ya samawi,

zambarau na nyekundu. Katikati ya matunda kulikuwa kengele. Yesu

ni mwenye kuzaa tunda katika ufufuko wake. Kengele linatukumbusha

faida ya ushuhuda wake.

Juu ya joho kulikuwa efodi kuvaa juu ya mabega na kwa mbavu

yake. Ilikuwa vilevile na mkaba wake. Ilisokotwa vizuri na umalidadi

wa nyuzi za samawi, zambarau na nyekundu pamoja na uzi wa zahabu.

Juu ya mabega kulikuwa vito viwili vya shohamu. Walichora juu ya

vito hivi majina ya wana wa Israeli. Vito vilifungwa katika vijalizo vya

zahabu. Hivi kila mara Haruni alipotokea mbele ya Mungu, alibeba

majina ya watu wa Mungu. Vivyo hivyo, Kuhani letu Mkubwa

anapeleka majina yetu kwa uwezo wa mabega yake mbele ya Mungu

Mtakatifu. Tunakumbuka Mchungaji Mwema akibeba kondoo

Kuhani Mkubwa 55

Page 56: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

mpotevu juu ya bega lake wakati alipomkuta, pahali pa amani na

salama.

Kwa kifua kuhani alibeba vito 12 katika mfuko wa umalidadi

wenye rangi. Kulikuwa kito kimoja kwa kila kabila la Israeli, kila kito

na jina lake. Tunawaza juu ya Yesu, Kuhani letu anayelinda majina

yetu, sisi watu wake, karibu na moyo wake wa mapendo.

Kulikuwa kilemba kama kofia na bamba la zahabu safi kuhani ali-

yobeba kwa paji la uso. Juu ya bamba hili, kwa kuchora, kulikuwa

mhuri, TAKATIFU KWA BWANA. Haruni alisimamia utakatifu wa

Israeli mbele ya Mungu. Kristo anasimamia utakatifu wa Kanisa lake

(2 Wakorinto 5:21).

Namna Mungu zamani alivyoona watoto wa Israeli katika mavazi

matakatifu na ya umalidadi wa Haruni, vivyo hivyo Mungu anatu-

tazama ndani ya Kristo, Kuhani letu mkubwa, katika mali ya neema

yake na uzuri wake wote.

Sisi waamini tunapata njia wazi kuingia Pahali Patakatifu kwa

damu ya Yesu. Mungu anatuita kumkaribia bila woga kama makuhani

yake waliosafishwa na damu ya sadaka iliyokubaliwa pia.

“Tuna uhodari wa kuingia Pahali Patakatifu kwa damu ya Yesu,

njia ile aliyoanza kwa ajili yetu, mpya, na hai, katika pazia, ndio mwili

wake; na tukiwa na kuhani mkubwa juu ya nyumba ya Mungu; tukari-

bie kwa moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, mioyo yetu ikikwisha

kunyunyiziwa kwa kuacha zamiri mbaya” (Waebrania 10:19-22).

“Basi, tukaribie kiti cha neema pasipo woga, ili tupewe rehema,

na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji” (Waebrania 4:16).

56 MIFANO YA KRISTO

Page 57: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

DAUDI NA KRISTO

Mungu alituma nabii Samweli kutaja mtu atakayekuwa mfalme wa Is-

raeli. Kwa mji wa Betelehemu, Samweli aliita watoto wa Yese

kuonekana mbele yake mmoja mmoja.

Wote wakatokea ila Daudi, mtoto aliyekuwa akilinda kondoo.

Samweli alitaka kuchagua Eliabu, mwana wa kwanza, lakini Mungu

alimwambia, “Usiangalie use wake, wala urefu wa mwili wake; kwa

maana nimemkataa. Kwa maana Bwana haoni kama mtu anavyoona,

maana mtu anaangalia kuonekana kwa inje, lakini Bwana anatazama

moyo” (1 Samweli 16:1-13).

Wakamwita Daudi. Mungu alimwagiza nabii, “Simama umpakae;

kwa maana huyu ni yeye. Halafu Samweli akachukua pembe ya

mafuta, akampakaa kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana alikuja na

uwezo juu ya Daudi tangu siku ile” (1 Samweli 16:12-13). Mungu

akachagua Daudi, mtumishi wake, akamwondoa katika mazizi ya ko-

ndoo (Zaburi 78:70).

Kristo alizaliwa kwa uzazi wa Daudi kwa njia ya mama yake (Luka

1:31-32). Yeye ni Mwana wa Mungu, Mchaguliwa mwenye heshima

(1 Petro 2:6).

Maana ya “Kristo” ni “Mpakaliwa.” Wakati Yesu alipobatizwa

katika Yorodani, kwa kutoka mtoni, Roho ya Mungu alimshukia kwa

sura ya hua. Mungu alimshuhudia akipaza sauti toka mbinguni

akisema, “Wewe ndiwe Mwana wangu, mpendwa wangu, ninape-

ndezwa nawe” (Marko 1:11).

Daudi alipakaliwa na mafuta (sura ya Roho Mtakatifu) kuonyesha

ya kuwa yeye ni mfalme wa watu wa Mungu duniani (Waisraeli).

Vivyo hivyo Mwana wa Mungu aliyezaliwa kwa mbegu ya Mfalme

Daudi alionyeshwa kuwa Kristo Mpakaliwa. Yeye ni Kichwa cha watu

wa Mungu, wenyeji wa mbingu.

57

Page 58: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

Daudi alichaguliwa kutawala ufalme wa taifa la dunia. Ali-

pakaliwa ajulikane kuwa mfalme, akitumika kwa uwezo wa roho ya

Mungu (1 Samweli 16:13). Roho ya Mungu alishukia Kristo aliye-

chaguliwa na Mungu kuwa Mfalme wa wafalme na Bwana ya wa-

bwana (Matendo 4:26-28; Ufunuo 19:11-16). Yeye ana ufalme usio na

mwisho.

Ndugu zake Daudi walimbeua (1 Samweli 17:28). Vivyo hivyo

ndugu zake Yesu hawakumwamini (Yoane 7:5; Marko 6:26; Yoane

1:11; Luka 9:22).

Daudi, akitaja jina la Yehova, alishindana na adui Goliata. Ali-

mshinda na kitu cha uzaifu, ndilo jiwe (1 Samweli 17:49-50).

Bwana Yesu Kristo alishinda adui Shetani na kitu cha uzaifu ndiyo

mauti ya msalaba. Tunasoma, “Kwa njia ya kufa apate kuharibu yeye

aliyekuwa na nguvu za kufa, ndiye Shetani, na kuwafungua wale wote

waliokuwa maisha yao yote katika hali ya utumwa, kwa woga wa

mauti” (Waebrania 2:14-15).

Wakati Daudi alipokataliwa na kuzarauliwa, alijiondosha katika

mji, akijificha ndani ya pango la Adulamu. Watu wachache walitoka

mjini wakimfikia na kuambatana naye pangoni (1 Samweli 22:1-2).

Vivyo Kristo sasa ni inje ya kambi ya dunia. Hashikamani na hali

ya ulimwengu wa sasa. Kazi ya Roho Mtakatifu sasa ni kuita watu ku-

toka katika dunia ya uovu kujitenga, kuwa kundi kwa jina lake. Hii ni

“eklesia” ndilo Kanisa la watu wanaotoka kukuta Yesu inje ya kambi

(Matendo 15:14).

Soma Yoane 17:14-17 na Yoane 15:19. Watu wa dunia wali-

chukia Yesu; watatuchukia sisi. “Twende kwake inje ya kambi, tu-

kichukua laumu lake” (Waebrania 13:13).

Daudi amefanana na Kristo kwani alikuwa mlinzi wa kondoo

(1 Samweli 16:11; 17:15). Alipiga vita kuponyesha kondoo zake kwa

adui simba na dubu (1 Samweli 17:34-36).

Bwana Yesu alijiita mwenyewe Mchungaji Mwema. Alijitoa kwa

ajili ya kondoo zake, ndio watu wake (Yoane 10:11,14). Kwa kufa

kwake anapatia kondoo zake uzima wa milele.

Kwa Luka 15:4-7 tunasoma juu ya mchungaji anayetafuta kondoo

58 MIFANO YA KRISTO

Page 59: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

yake mpotevu. Akimkuta akafurahi na shangwe. Mbingu inajaa furaha

wakati mwenye zambi anapotubu, akiponyeshwa na Kristo, Mchun-

gaji Mwema.

Tulikuwa tukipotea kama kondoo, lakini sasa tumerudi kwa

Mchungaji na Mwangalizi wa roho zetu. (Tazama 1 Petro 2:25).

Tupendane na Mwokozi Yesu sasa kwa wakati wa kukataliwa

kwake kama Yonatana alivyopendana na Daudi. Yonatana alikuwa na

mapatano na Daudi kwa kuwa alimpenda kama nafsi yake mwenyewe.

Yonatana aliondosha vazi alilovaa, akampa Daudi, na nguo zake, hata

upanga wake na upindi wake na mshipi wake (1 Samweli 18:3-4).

Yonatana akapendezwa sana na Daudi (1 Samweli 19:2), akasifu

Daudi (1 Samweli 19:4) , akamwambia Daudi, “Kitu gani nafsi yako

inachotaka nitakufanyia” (1 Samweli 20:4).

Mungu atupe roho namna ya Yonatana mbele ya Daudi hata sisi

tupendane na Kristo hivi. Tuwe tayari kutoa vitu vyetu vyote mbele

yake na kumwambia, “Nitafanya vitu vyote unavyovitaka nifanye.”

Hivi mapenzi yake yatatutawala na mapatano yetu na Kristo yatahaki-

kishwa katika matendo ya mapendo.

Daudi na Kristo 59

Page 60: MIFANO YA KRISTO - Everyday Publications Inc. Titles cha Zahabu 45 Meza ya Mkate wa Onyesho 47 Mazabahu ya Kuchoma Uvumba 49 Pazia, Sanduku ya Agano na Kiti cha Rehema 51 Kuhani Mkubwa

JUMLISHO

Tumefika kwa mwisho wa kitabu hiki. Tumepata mifano mingi katika

Agano la Kale juu ya Bwana Yesu. Wakati tunaposoma Agano Jipya,

tunafahamu namna mifano hii inafanana na Mwokozi wetu. Hivi tu-

napata masawanisho na maelezo juu ya hali ya Bwana na maisha yake

na mauti yake.

Tusikwame juu ya vivuli, tuendelee kwa maana ya kweli katika

Yesu mwenyewe. Waebrania 10:1 linasema, “Basi kwa kuwa torati ni

kivuli cha yale mema yatakayokuwa, wala si sura yao yenyewe.” Tu-

endelee mbele, kufahamu maana ya torati na vivuli vingine kupata

maana ya kweli ndani yao juu ya Bwana Yesu aliyefika duniani, si

kuharibu torati, lakini kuitimiza. (Soma Matayo 5:17).

Kuna mifano mingi mingine katika Agano la Kale inayofanana na

Yesu. Yona, kukaa ndani ya samaki siku tatu na usiku tatu, anafanana na

Yesu katika kaburi (Matayo 12:40). Boazi wa jamaa ya bwana yake Ruta

anafanana na Yesu aliyejifananisha kuwa mtu akomboe Kanisa, tuwe

bibi yake (Ruta 4:1,6,9,10). Kamba nyekundu Rahaba aliyofunga juu ya

ukuta wa Yeriko kwa kujiponyesha na jamaa yake inatuku-mbusha juu

ya damu ya Yesu kutupatia wokovu na amani (Yosua 2:21; 6:17, 25).

Hata mawe 12 yaliyowekwa ndani ya Yorodani wakati Waisraeli

walipovuka ngambo kwa inchi kavu ni sura ya Mwokozi Yesu akizama

chini ya gazabu ya Mungu msalabani. (Tazama Zaburi 42:7). Waisraeli

walipanga mawe mengine 12 kwa pwani kando ya Yorodani katika

Kanana. Mawe 12 ndani ya mto yalikomboa mawe 12 ya kupona kwa

pwani ya Yorodani. Sura ya ukombozi wa Kristo kwa watu wake!

Mbele ya mambo haya, wakati wa kusafiri kwa Waisraeli ja-

ngwani, walifika kwa maji machungu “Mara.” Walikuwa na kiu lakini

hawakuweza kunywa maji pale. Walinungunika juu ya Musa. Yeye

aliomba Mungu. Alimwonyesha mti. Wakati Musa alipotupa mti ule ndani

ya maji machungu yaligeuka matamu. Watu wakakunywa, wakapona. Pale

tunapata sura ya msalaba — kuleta uzima badala ya mauti.

Biblia inajaa na maneno mazuri mazuri — kama hazina ya damani.

Tutafutetafute ndani yake kupata mali kufurahisha roho zetu na roho za

wengine kwa utukufu wa Mwokozi wetu Yesu Kristo.

60